Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Mbinu 3 Rahisi Zitakazokusaidia Na Kufanya Wateja Wakupende Bila Kujipendekeza…

 ‎

‎Kakaa/Dadaa....

‎Unajua shida kubwa ya wauzaji wengi ni nini?

‎Wanahangaika kuwafanya wateja wawapende…

‎Wanawafuata wateja kila kona…

‎Wanaomba omba mapenzi kama wahitaji…

‎Lakini bado…

‎Wateja hawawaoni!

‎Wateja hawawakumbuki!

‎Wateja hawasikii hata huruma!

‎Mbaya zaidi, kuna jamaa mwingine hajawahi hata kujitambulisha sana…

‎Lakini kila mteja anamuita, anamfuata, anamwamini!

‎Unajiuliza… *Kwa nini sio mimi?*

‎Kwa nini mimi ndo napigwa chenga kila siku?

‎Ngoja nikuambie kitu cha ukweli…

‎Wateja hawapendi mtu anayeomba sana.

‎Wanapenda mtu anayewaonyesha thamani… kimya kimya.

‎Na ndo maana leo nakupa hizi mbinu 3.

‎Mbinu za mtaa.

‎Rahisi sana… lakini zenye uzito wa almasi.

‎MBINU #1: Usijiuze, Jionyeshe

‎Acha kulalamika eti watu hawakunotisi…

‎Wewe jionyeshe tu kwa vitendo.

‎Jibu comment zao.

‎Watumie ujumbe unaosaidia bila kutegemea chochote.

‎Toa msaada mdogo mdogo kwenye status zako.

‎Wacha maneno mengi.

‎Tenda.

‎Waonyeshe kuwa upo… bila kuomba.

‎Wateja hupenda watu wanaojituma kimya kimya.

‎MBINU #2: Wasaidie Bila Hata Kuombwa.

‎Siku hizi watu wamechoka na wauzaji wanaoshika shika mabega.

‎Wanataka mtu anayejua shida zao kabla hawajasema.

‎Ukiona mtu analalamika hana wateja…

‎Mtumie voice note moja ya sekunde 15 ya motisha.

‎Ukiona mtu anahangaika na bei…

‎Mtumie tips 3 za kuongeza faida bila kuongeza bei.

‎Unajua nini?

‎Atasave jina lako.

‎Atakutafuta mwenyewe.

‎Kwa sababu ulimgusa… bila kuomba.

‎MBINU #3: Jenga Hadithi Yako Kwenye Maisha Yao

‎Watu wanapenda mtu anayejua walikotoka.

‎Mtu anayewakumbusha maisha yao.

‎Mtu anayewaelewa bila hukumu.

‎Ukitangaza bidhaa, weka kisa.

‎Kisa cha mtu aliyewahi kuwa na tabu… lakini bidhaa yako ikambadilisha.

‎Kisa ambacho wao wanaweza sema, “Dah, huu ni mimi kabisa!”

‎Ukifanya hivi…

‎Utakua si muuzaji tena…

‎Utakua rafiki yao.

‎Na marafiki wanapendwa bila kuomba!

‎SASA SKIZA HII HADITHI FUPI (Real Story)

‎Kuna kijana mmoja anaitwa Musa.

‎Alikua anauza sabuni za mikono.

‎Kila siku alikua anapost, *Beba yako leo…!*

‎Hakuna aliyecomment.

‎Hakuna aliyejibu.

‎Siku moja, akabadili mbinu…

‎Aliandika hivi:

‎“Dada yangu alinipigia simu akilia, mikono yake imejaa mipasuko kwa kutumia sabuni za kawaida. Nikamtumia hii sabuni yangu… ndani ya wiki 1, akaniambia: *Musa, mikono yangu imekuwa kama ya mtoto.*

‎Ndo hapo nikajua… watu hawauzi bidhaa, watu huuza matokeo.

‎Baada ya post hiyo…

‎Watu 57 walimuinbox.

‎28 walinunua siku hiyo hiyo.

‎Leo hii Musa hana muda wa kusaka wateja.

‎Wateja wanamsaka yeye.

‎Kwa nini?

‎Kwasababu....

‎Aliwafanya wampende… bila kuomba.

‎Sasa ni zamu yako.

‎Acha kuomba.

‎Acha kukimbizana.

‎Fanya haya matatu…

‎Na utaona maajabu.

‎Ukihitaji msaada, Piga au Tuma Meseji NAMBA Ni 0750376891.

‎Lakini ukitekeleza hizi mbinu 3…

‎Wateja watapiga hodi kwenye inbox yako kila siku!

‎Karibu.

‎0750376891.

‎Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection