Machapisho

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Acha Kuomba Anza Kuitwa….

Picha
Rafiki Yangu, Miaka mitatu (3) iliyopita, Nilikutana na kijana mmoja ambaye aliniambia,  “Kaka, mimi huandika inbox 50 kwa siku hakuna anayejibu.  Wengine hata huniblock.” Nilimtazama kwa upole nikamwambia,  “Labda tatizo si watu ni wewe kuomba badala ya kuvutia.”  Siku hizi biashara si ya kuomba omba huruma, ni ya kujijenga kiasi kwamba watu wenyewe wanakuja kukuomba uwauzie.  Uliposikia kuhusu kampuni kama Apple, walikuita au uliwakimbilia?  Ndiyo maana leo tunasema: acha kuomba anza kuitwa. Somo hili utajifunza. Jinsi ya kuacha kuomba wateja bila mafanikio, Njia za kujijenga ili wateja wakutafute wenyewe, Mbinu za kuvutia badala ya kusumbua,Mitazamo mipya ya kibiashara inayokufanya uonekane wa thamani kubwa. Fikiria ukiamka asubuhi na unakuta ujumbe: "Habari, nimesikia kuhusu huduma yako, naomba unisaidie… "Watu wanaku-tag mitandaoni, wanakutumia referrals, wanakutafuta wenyewe.  Umeacha kusukuma watu sasa unavutia kwa nguvu.  Unapumua kwa raha...

‎Jinsi ya Kutumia Kitabu Kuanzisha Biashara Yenye Misingi Imara Bila Hatari Kubwa...

 ‎*Jinsi ya Kutumia Kitabu Kuanzisha Biashara Yenye Misingi Imara Bila Hatari Kubwa*... ‎ ‎Rafiki Yangu, ‎ ‎Kila shujaa anaanza na ndoto kubwa… ‎Lakini mara nyingi ndoto hizo hukwama kwa hofu. ‎ ‎Labda na wewe umewahi kujiuliza: ‎ ‎“Nitanzaje biashara yangu?  ‎ ‎Sitapoteza pesa nyingi?  ‎ ‎Wateja watanipokea kweli?” ‎ ‎Kwa wengi, ndoto ya biashara hubaki kichwani kwa sababu ya hofu ya kushindwa, mtaji mdogo, na ukosefu wa mwelekeo. ‎ ‎Ndiyo maana wengi huchelewa kuanza, au huanza vibaya na kufeli mapema. ‎ ‎👉 Lakini safari ya shujaa huanza pale anapogundua njia mpya. ‎ ‎Hapo ndipo Hamisi kutoka Dodoma alipoamua kuwa shujaa wa maisha yake. ‎ ‎Hamisi alikuwa kijana mwenye ndoto ya kuuza bidhaa za asili.  ‎ ‎Alikuwa na shauku kubwa, lakini hana mtaji mkubwa. ‎ ‎Kila mara alipoketi kufikiria biashara yake, hofu ya kupoteza pesa ilimrudisha nyuma. ‎ ‎Mpaka siku moja, aliposoma The Lean Startup cha Eric Ries. ‎ ‎Ndipo akagundua mbinu ya kipekee: Tumia kitabu kama chombo c...

‎Jinsi Ya Kusoma Dakika 5 Na Kuchukua Pointi 10 Zitakazobadilisha Maisha Yako...

Picha
‎ Rafiki Yangu Mpendwa, ‎ ‎Kumbuka.... ‎ ‎Kila shujaa ana changamoto anayoipigania… ‎ ‎Na labda yako ni hii: ‎ ‎Unachukua kitabu kizuri mikononi, unaanza kusoma kwa hamasa kubwa. ‎ ‎Lakini dakika chache baadaye, macho yanachoka, akili inazurura, na unajikuta unasoma bila kuelewa chochote. ‎ ‎Mwisho wa siku, unasema: *Sina muda wa kusoma vitabu hivi kwa kweli.* ‎ ‎❌ Hapo ndipo ndoto nyingi za kupata maarifa na kubadilisha maisha zinakufa. ‎ ‎Lakini safari ya shujaa haishii hapo. ‎ ‎👉 Hapa ndipo siri ya Mortimer Adler kwenye kitabu chake cha How to Read a Book inapoingia. ‎ ‎Kuna mbinu rahisi sana ya kubadilisha hali hiyo: Soma Dakika 5 Pekee, Chukua Pointi 10. ‎ ‎Na kuna shujaa mmoja wa mtaani, Anayeitwa Juma kutokea Sinza, ‎ ‎Alijifunza mbinu hii. ‎ ‎Juma alikuwa mfanyabiashara mdogo wa kuuza chakula sokoni. ‎ ‎Alitaka kuboresha maisha yake na biashara, lakini hakupata muda wa kusoma vitabu vikubwa. ‎ ‎Alijaribu mara nyingi, lakini kila mara alishia kati...

‎*Safari ya Shujaa: Jinsi Ya Kuvunja Vikwazo Vya Kusoma Na Kumaliza Kila Kitabu Bila Kukata Tamaa... ‎

Rafiki Yangu, ‎ ‎Kila shujaa ana safari yake ya kipekee. ‎Na safari yako inaweza kuanza na kitabu. 📖 ‎ ‎Lakini ukweli ni huu… ‎ ‎Mara nyingi unapochukua kitabu, unaanza kwa nguvu. ‎ ‎Lakini baada ya kurasa chache, akili yako inachoka. Simu inaita. Mawazo yanakukimbia. ‎ ‎Na ndoto ya kumaliza kitabu inapotea kama upepo. ‎ ‎Hii ndiyo changamoto kubwa ya wasomaji wengi, ‎ ‎...kuanza kwa ari, lakini kukwama katikati. ‎ ‎Lakini hapa ndipo safari ya shujaa inaanza. ‎ ‎Amina, msichana wa kawaida kutoka Mbagala, alitaka sana kubadilisha maisha yake kupitia vitabu. ‎ ‎Kila mara alipojaribu, alijikuta anakwama , akili inachoka, mazingira yenye vurugu. ‎ ‎Alikaribia kuacha kabisa… ‎ ‎Mpaka siku moja, alipokutana na mbinu 3 rahisi kutoka kwa Neil Fiore kwenye kitabu chake cha The Now Habit. ‎ ‎Alijifunza kuanza na dakika 15 tu, kuweka malengo madogo, na kujenga mazingira safi ya kusoma. ‎ ‎Matokeo? ‎Ndoto yake ya kumaliza vitabu ikawa kweli. ‎ ‎Sasa anasoma, anafurahia, anakumbuka na kutumia maar...

‎Stori; Kila Unachotafuta Kimeandikwa Tayari...

Hii hapa ni ile stori ya mama wa watoto Wawili... ‎ ‎Halima, mama wa watoto wawili kutoka Mbeya, alianza biashara ndogo ya *breakfast café* ‎ ‎Alikuwa na ndoto kubwa, lakini baada ya miezi mitatu wateja wakapungua. ‎ ‎Kila jioni aliuliza nafsi yake: *Labda chakula changu si kizuri… au sijui kutangaza?* ‎ ‎Akawa amechoka, amechanganyikiwa, na karibu akate tamaa. ‎ ‎Siku moja rafiki yake alimpatia kitabu: ‎📘 Awaken the Giant Within – Tony Robbins. ‎ ‎Halima hakuamini sana. Alisema: *Kitabu kitanisaidia kweli?* ‎ ‎Lakini akahisi sauti ikimnong’oneza: “Jaribu, hakuna cha kupoteza.” ‎ ‎Aliposoma sura chache, aligundua kuwa tatizo halikuwa chakula chake… ‎ ‎Ilikuwa mpangilio wa huduma na kukosa promosheni. ‎ ‎Akachukua hatua ndogo: ‎ ‎Akaandika menyu mpya yenye “grab-and-go.” ‎ ‎Akawapa punguzo wateja wa kwanza. ‎ ‎Akashirikiana na maduka jirani kwa promosheni. ‎ ‎Mara ya kwanza haikuwa rahisi, alihisi woga, lakini aliendelea kutekeleza. ‎ ‎Ndani ya miezi miwili, mauzo yalipanda kwa 70%. ‎ ...

Kwa Nini Wateja Wako Wanaonyesha Nia Lakini Hawanunui? (Na Siri ya NDOANO YA KISASA Inavyowageuza Kuwa Wanunuzi Haraka)

Rafiki Yangu, ‎ ‎Kulikuwa na mfanyabiashara mmoja, jina lake Halima. ‎Alikuwa na bidhaa nzuri mno, kila mtu aliyekuja dukani kwake alisifia. ‎Lakini tatizo moja kubwa lilikuwa linamtafuna usiku na mchana: ‎ ‎👉 Wateja wengi walionyesha nia… walipiga maswali mengi… walionekana wamekaribia kununua… ‎Lakini mwisho wa siku, waliondoka bila kufanya maamuzi. ‎ ‎Halima alihisi kama anapanda mbegu nzuri kwenye ardhi yenye rutuba… lakini mazao hayatokei. ‎Alijiuliza: “Hivi shida ipo kwao au ipo kwangu?” ‎ ‎Siku moja, Halima alipata rafiki aliyemwambia: ‎“Hii sio juu ya bidhaa yako pekee. Ni juu ya ndoano unazotumia kuwashawishi.” ‎ ‎Alimshauri achukue kitabu kipya kinachoitwa: ‎📘 NDOANO YA KISASA – Sanaa ya kuwageuza wale wanaoonyesha nia kuwa wanunuzi wa kudumu. ‎ ‎Halima hakuamini mara moja. Alifikiri, “Vitabu tena? Mimi nahitaji wateja sasa hivi!” ‎Lakini moyo wake ulisema: “Jaribu, hakuna cha kupoteza.” ‎ ‎Akiwa na wasiwasi, alianza kusoma ukurasa baada ya ukurasa. ‎Kila ukurasa ulikuwa ka...

‎Hivi Ndivyo Matajiri Wanavyokula Vitabu.... ‎

‎Siri Moja Inayowafanya Matajiri Kufanikisha Ndoto Zao Haraka Na Kwa Urahisi.... ‎ ‎Rafiki Yangu, ‎ ‎Je, unajua kuwa wengi wanaotaka kuwa matajiri wanashindwa kwa sababu hawajui siri moja rahisi ambayo matajiri wakuu wote wanaizingatia? ‎ ‎Je, unajua siri hiyo ipo kwenye vitabu, na kila tajiri mkubwa anaitumia kila siku? ‎ ‎Changamoto kubwa kwa wengi ni kutokuwa na mtazamo wa mafanikio unaoendana na yale waliyosoma au kujifunza. ‎ ‎Wengi hujifunza mitazamo mibaya kuhusu pesa, mafanikio, na hata mafanikio na maisha kwa ujumla. ‎ ‎Wanadhani kuwa na utajiri ni bahati tu, au ya wale walio na bahati kwa hali ya ajabu. ‎ ‎Wanajikuta wakifanya kazi ngumu bila mkakati, wanapoteza muda na pesa katika njia zisizo na tija. ‎ ‎Tatizo ni kwamba hawajui kuwa kuna siri moja kuu ya mafanikio iliyojificha ndani ya vitabu vya maarifa, na hiyo ni kusoma kwa mwelekeo sahihi na kutumia maarifa hayo kuunda mtazamo wa utajiri. ‎ ‎Kumekuwepo na dada mmoja aitwaye Amina kutoka Kariakoo, Dar es Salaam. ‎ ‎Amina...