Jinsi ya Kutumia Kitabu Kuanzisha Biashara Yenye Misingi Imara Bila Hatari Kubwa...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
*Jinsi ya Kutumia Kitabu Kuanzisha Biashara Yenye Misingi Imara Bila Hatari Kubwa*...
Rafiki Yangu,
Kila shujaa anaanza na ndoto kubwa…
Lakini mara nyingi ndoto hizo hukwama kwa hofu.
Labda na wewe umewahi kujiuliza:
“Nitanzaje biashara yangu?
Sitapoteza pesa nyingi?
Wateja watanipokea kweli?”
Kwa wengi, ndoto ya biashara hubaki kichwani kwa sababu ya hofu ya kushindwa, mtaji mdogo, na ukosefu wa mwelekeo.
Ndiyo maana wengi huchelewa kuanza, au huanza vibaya na kufeli mapema.
👉 Lakini safari ya shujaa huanza pale anapogundua njia mpya.
Hapo ndipo Hamisi kutoka Dodoma alipoamua kuwa shujaa wa maisha yake.
Hamisi alikuwa kijana mwenye ndoto ya kuuza bidhaa za asili.
Alikuwa na shauku kubwa, lakini hana mtaji mkubwa.
Kila mara alipoketi kufikiria biashara yake, hofu ya kupoteza pesa ilimrudisha nyuma.
Mpaka siku moja, aliposoma The Lean Startup cha Eric Ries.
Ndipo akagundua mbinu ya kipekee: Tumia kitabu kama chombo cha kuanzisha biashara.
🌟 Hapo ndipo mabadiliko yake yalianza.
Hamisi aliandika kijitabu kidogo kuhusu faida za bidhaa zake.
Akaanza kukiuza na kukisambaza kwa watu wachache, si kwa lengo la kupata faida kubwa, bali kupata mrejesho wa kweli.
Na kilichotokea kilimshangaza:
Watu walipendezwa na elimu aliyoshirikisha,
Walitoa maoni ya kuboresha bidhaa,
Na wengi waligeuka kuwa wateja wa kudumu.
Hamisi hakupoteza pesa nyingi, hakusubiri miaka, hakuhangaika bila mwelekeo.
Alitumia kitabu kidogo kama daraja la kuanzisha biashara halisi.
Sasa, biashara yake inakua kwa kasi, ikiheshimika Dodoma na hata mikoa ya jirani.
Na sasa ni nafasi yako kuanza safari yako.
👉 Leo, fanya hatua moja ndogo:
Andika wazo kuu la biashara yako,
Andika ukurasa au sura ndogo ya kitabu inayobeba suluhisho lako,
Shiriki na watu wachache kupata mrejesho wa kweli.
Kumbuka: Haujengi biashara kwa kuwekeza mamilioni mara moja,
... unajenga kwa hatua ndogo, zenye busara, na msingi thabiti.
Anyway, Kama Bado Hujapata Kitabu Kipya Cha NGUVU Ya Kitabu,
Piga au Tuma Ujumbe "NGUVU YA KITABU" Kwenda 0755376891.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Mwandishi| Mkufunzi| Kocha.
0755376891.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni