Acha Kuomba Anza Kuitwa….
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu,
Miaka mitatu (3) iliyopita,
Nilikutana na kijana mmoja ambaye aliniambia,
“Kaka, mimi huandika inbox 50 kwa siku hakuna anayejibu.
Wengine hata huniblock.” Nilimtazama kwa upole nikamwambia,
“Labda tatizo si watu ni wewe kuomba badala ya kuvutia.”
Siku hizi biashara si ya kuomba omba huruma, ni ya kujijenga kiasi kwamba watu wenyewe wanakuja kukuomba uwauzie.
Uliposikia kuhusu kampuni kama Apple, walikuita au uliwakimbilia?
Ndiyo maana leo tunasema: acha kuomba anza kuitwa.
Somo hili utajifunza.
Jinsi ya kuacha kuomba wateja bila mafanikio,
Njia za kujijenga ili wateja wakutafute wenyewe,
Mbinu za kuvutia badala ya kusumbua,Mitazamo mipya ya kibiashara inayokufanya uonekane wa thamani kubwa.
Fikiria ukiamka asubuhi na unakuta ujumbe:
"Habari, nimesikia kuhusu huduma yako, naomba unisaidie…
"Watu wanaku-tag mitandaoni, wanakutumia referrals, wanakutafuta wenyewe.
Umeacha kusukuma watu sasa unavutia kwa nguvu.
Unapumua kwa raha, biashara inatiririka kama maji.
Ndoto ya kila mfanyabiashara ni kuitwa na hiyo ndoto inaweza kuwa kweli, kuanzia leo.
Mimi mwenyewe nilianza kama muombaji.
Nilikuwa naandika hadi watu wananiita “msumbufu.
” Lakini nilipogundua kuwa mvuto huzalishwa kwa njia ya thamani, nilibadilika.
Nilianza kutoa elimu ya bure, kushiriki uzoefu wangu, kusikiliza shida za watu.
Miezi mitatu baadaye, inbox yangu ilianza kubadilika.
Watu walikuwa wakiniambia, “Nimekuwa nikikufuatilia muda mrefu naomba unisaidie.
” Ndiyo nguvu ya kuitwa.
Njia 5 Za Kuhakikisha Wateja Wanaanza Kukuita…
1. Jenga Thamani Inayoonekana:
Toa elimu. Andika, ongea, rekodi video.
Watu wanavutwa na watu wanaowasaidia hata kabla hawajawalipa.
Kama huoneshi unachojua, usitarajie waje kukuuliza.
2. Kuwa Suluhisho, Siyo Muuzaji:
Badala ya kusema “nauza sabuni,” sema “nasaidia akina mama kuondoa madoa bila sumu.”
Hii inaweka akili ya mteja kwenye suluhisho, si bei.
3. Jenga Mvuto Wa Kitaaluma (Professional Pull):
Fanya kazi kwa ubora hata kama ni kwa mteja mmoja.
Akitoka akisema “huyu mtu ni wa tofauti,” atakuletea wengine bila kusema.
4. Shirikiana Na Watu Wenye Jamii (Collaboration):
Jifunze kushirikiana badala ya kushindana.
Tafuta mtu mwenye jamii tayari (mtu wa mitandao, mwalimu, mshauri) mshirikiane na tafuta nafasi ya kujitambulisha bila kuuza moja kwa moja.
5. Kuwa Hai Kwenye Maeneo Ambayo Wateja Wapo:
Kama wateja wako wako WhatsApp, jenga broadcast list.
Kama wako Telegram, fungua group. Kama wako TikTok, toa elimu fupi.
Usiogope kuonekana mara kwa mara uvutano hutokea kupitia “exposure.
”Leo, simama kwenye ukweli: kuomba ni mzigo.
Kuvutia ni mteremko. Anza kujenga mvuto wako:
Chagua jukwaa moja la kuonyesha thamani yako kila siku,
Tengeneza mfumo wa kukusanya ushuhuda wa wateja,
Na kama Bado leo, anza kuitengeneza.
Anyway, kama bado hujapata kitabu kipya Cha NDOANO YA KISASA,
Na kile cha NGUVU YA KITABU,
Unajipunja.
Piga simu sasahivi, Kwenda 0755376891.
Kisha utapewa.
Kutoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Mwandishi| |Copywriter| Mkufunzi| Kocha.
0755376891
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

Maoni
Chapisha Maoni