*Safari ya Shujaa: Jinsi Ya Kuvunja Vikwazo Vya Kusoma Na Kumaliza Kila Kitabu Bila Kukata Tamaa...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu,
Kila shujaa ana safari yake ya kipekee.
Na safari yako inaweza kuanza na kitabu. 📖
Lakini ukweli ni huu…
Mara nyingi unapochukua kitabu, unaanza kwa nguvu.
Lakini baada ya kurasa chache, akili yako inachoka. Simu inaita. Mawazo yanakukimbia.
Na ndoto ya kumaliza kitabu inapotea kama upepo.
Hii ndiyo changamoto kubwa ya wasomaji wengi,
...kuanza kwa ari, lakini kukwama katikati.
Lakini hapa ndipo safari ya shujaa inaanza.
Amina, msichana wa kawaida kutoka Mbagala, alitaka sana kubadilisha maisha yake kupitia vitabu.
Kila mara alipojaribu, alijikuta anakwama , akili inachoka, mazingira yenye vurugu.
Alikaribia kuacha kabisa…
Mpaka siku moja, alipokutana na mbinu 3 rahisi kutoka kwa Neil Fiore kwenye kitabu chake cha The Now Habit.
Alijifunza kuanza na dakika 15 tu, kuweka malengo madogo, na kujenga mazingira safi ya kusoma.
Matokeo?
Ndoto yake ya kumaliza vitabu ikawa kweli.
Sasa anasoma, anafurahia, anakumbuka na kutumia maarifa yake kuboresha biashara na maisha.
🌟 Huo ndio ushindi wa shujaa.
Na sasa ni zamu yako.
👉 Leo, chukua hatua ndogo kama shujaa:
Chagua kitabu
Weka dakika 15 tu
Tafuta sehemu tulivu
Hapo ndipo safari yako ya kusoma na kumaliza kila kitabu kwa urahisi inaanza.
Kumbuka: Kila shujaa anaanza na hatua moja ndogo.
Anza na kitabu kipya Cha *NGUVU YA KITABU*
Kukipata tuma Meseji "NGUVU YA KITABU"
Kwenda 0755376891.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Mwandishi| Mkufunzi| Kocha
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni