Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Utajiri Unaanza Na Dakika 15 Tu Kila Siku Na Hakuna Atakayekuanbia HILI!


‎‎Aliwahi kuwa maskini sana. Hakuwahi kumaliza hata kitabu kimoja maishani mwake.

‎Lakini siku moja, alijilazimisha kusoma dakika 15 tu kabla ya kulala.

‎Mwaka mmoja baadaye, alikuwa na biashara tatu, kipato cha kila siku, na uhuru aliokuwa akiuota.

‎Ni ajabu eeh?

‎Ndiyo.

‎Lakini si uchawi. Ni nguvu ya maarifa madogo kila siku.

‎Katika makala hii, nitakuonyesha jinsi dakika 15 tu za kusoma kila siku zinavyoweza kukutoa kwenye maisha ya kukopa hadi maisha ya kutajirika.

‎Nitakufundisha:

‎Nini cha kusoma

‎Jinsi ya kuanza

‎Na kwanini dakika 15 ni zaidi ya kutosha.

‎Fikiria maisha yako baada ya miezi 6:

‎Unaongea kwa ujasiri.

‎Unajua wapi pa kuwekeza.

‎Una wazo la biashara.

‎Unajua kutunza fedha zako.

‎Unajiamini zaidi.

‎Watu wanaanza kukuona tofauti.

‎Kila siku unakaribia mafanikio.

‎Na yote yalianza na kurasa chache tu kila jioni.

‎Watu maarufu kama Warren Buffett, Elon Musk, na Oprah Winfrey wamesema wazi “kusoma kila siku ndicho kilichowatengeneza.”

‎Buffett husoma kurasa 500 kila siku.

‎Lakini hakuanza hivyo.

‎Alianza kwa dakika chache.

‎Ndiyo maana leo anaendesha mabilioni ya dola.

‎Hata hapa nyumbani ,kuna vijana waliokuwa wamekata tamaa, lakini baada ya kuanza kusoma vitabu vya fedha, biashara na maendeleo binafsi maisha yao yalibadilika kama usiku na mchana.

‎Sasa hivi unaweza kusema: “Sina muda.”

‎Lakini ukweli ni huu: kila mtu ana dakika 15.

‎Badala ya kuperuzi mitandao bila mpango, geuza dakika hizo kuwa uwekezaji kwenye ubongo wako.

‎👉 Chagua kitabu kimoja tu kwa mwezi mfano: Nguvu Ya vitabu, Mwanafunzi wa Pesa, Rich Dad Poor Dad, au Think and Grow Rich.

‎👉 Soma kurasa 5 tu kila siku hata ukiwa umechoka.

‎👉 Chukua dondoo moja na uiweke kazini kesho.

‎Hakuna sharti umalize haraka muhimu ni kufanya kila siku.

‎Usiseme “Nitaanza kesho.”

‎Kesho huja na visingizio vipya.

‎Anza leo. Dakika 15 tu hakuna anayekuzuia isipokuwa wewe mwenyewe.

‎Chukua kitabu.

‎Soma kurasa chache.

‎Kesho rudia.

‎Mwezi ujao utaona tofauti.

‎Mwaka mmoja ujao utamshukuru sana “Wewe” wa leo.

‎Usitafute miujiza wewe ndiye muujiza.

‎Dakika 15 tu kila siku zinaweza kubadili jina lako kwenye orodha ya walalahoi hadi kwenye orodha ya wenye mafanikio.

‎Usikubali maisha yakupite bila wewe kuyatawala.

‎Dakika 15 Huo ndio mwanzo wa utajiri wako.

‎Anza leo.

‎Anyway, kama unataka vitabu vizuri basi piga simu 0750376891.

‎Karibu.

‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection