‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

 

‎Ukipitia hii, kumbukumbu zako zitakuwa kama za kasuku aliyefundishwa kuimba chorus ya Diamond...





‎Kakaa/Dadaa Yangu...


‎Unasoma kitabu leo…


‎Kesho haukumbuki hata ukurasa wa kwanza.


‎Ukiulizwa ulichojifunza, unazubaa kama umepigwa na butwaa.


‎Unajikuta unasoma tu ilimradi umalize, si kwa sababu unaelewa au utakumbuka.


‎Yani unatumia muda wako kusoma…


‎Unaweka akiba ya maneno kichwani…


‎Halafu akili inafuta kila kitu kama flash drive yenye virus!


‎Unasoma vitabu vingi, ila akili haina ushahidi wowote.


‎Inapoteza kumbukumbu kama ex wako aliyesahau yote mliyowahi kupitia.


‎Lakini mbona kuna wengine wakisoma, wanakumbuka hadi mistari ya mwisho?


‎Hii ndo pointi ya kukasirikia!


‎Sio kwamba Huna Akili.


‎Sio kwamba huna uwezo.


‎Ni mbinu tu unazotumia ndizo za kizamani.


‎Zile za kukariri bila kuelewa, au kusoma harakaharaka kama unakimbizana na deadline ya NECTA.


‎Zisahau. Hapa nakuletea mbinu mpya, za kisasa, na za uhakika.


‎Zikikupita, utabaki na kichwa kizito kisicho na content.


‎ Twende sasa… Hizi ndizo MBINU 7 ZA KUKUMBUKA UNACHOSOMA:


‎MBINU YA KWANZA:

‎Soma kwa Sauti

‎Usione aibu, jifunze kuongea na kitabu chako.


‎Ukisoma kimya kimya, akili inaweza kuwa inasafiri.


‎Soma kwa sauti hata sauti ya chini.


‎Itakusaidia kusikia, kuelewa, na kukumbuka.


‎Ni kama kuongea na rafiki, unaelewa zaidi.


‎MBINU YA PILI:

‎Fanya Summary kwa Maneno Yako

‎Ukimaliza sehemu fulani, simama.


‎Jisomee upya, lakini kwa maneno yako mwenyewe.


‎Hii inasaidia ubongo kushughulika kuchuja kilicho muhimu.


‎Na utakumbuka kwa muda mrefu zaidi.


‎MBINU YA TATU:

‎Fundisha Mtu Mwingine.


‎Ukisoma na ukaweza kumfundisha mwingine, basi umekielewa kweli.


‎Mchukue kaka, dada, rafiki au hata mpenzi wako…


‎Mwambie ulichosoma kama vile wewe ndiye mwandishi.


‎Trust me utakumbuka hadi footnote!


‎MBINU YA NNE:


‎Chora au Andika Pointi Muhimu.


‎Ubongo unakumbuka picha kuliko mistari.


‎Tengeneza ramani ya akili (mindmap), chora mistari, andika kwa rangi tofauti.


‎Hii inaleta rangi kwenye kumbukumbu zako na inazishikilia vizuri.


‎MBINU YA TANO: Tumia Hisia.


‎Gusa hisia zako unapokutana na pointi kali.


‎Kama inakugusa moyo, simama.


‎Jiulize: “Hii inamaanisha nini kwangu?”


‎Unapohusisha hisia na kusoma, kumbukumbu hujikita kwenye moyo.


‎Na moyo hausahau kirahisi.


‎MBINU YA SITA:


‎Rudia Mara kwa Mara.


‎Usisome mara moja tu halafu usubiri miujiza?


‎Hapana, bro!


‎Rudia tena na tena.


‎Kila ukirudia, unakumbuka zaidi.


‎Repetition is the mother of mastery.


‎MBINU YA SABA:


‎Tumia Wakati Bora wa Ubongo.


‎Asubuhi au usiku kabla ya kulala…


‎Ubongo unakuwa fresh na tulivu.


‎Usisome ukiwa na njaa au umechoka—hakuna kitakachokaa kichwani.


‎Tafuta muda ambapo akili yako iko active.


‎Hapo ndipo uweke content ya nguvu.


‎Kuna dogo mmoja anaitwa Musa.


‎Alikuwa ana penda sana kusoma vitabu.


‎Lakini alikuwa na tabu moja hakumbuki chochote.


‎Alisoma kitabu cha “NGUVU YA VITABU”

‎Wiki moja baadaye, hakuwa anakumbuka hata jina la kitabu.


‎Nilimfundisha hizi mbinu saba…


‎Baada ya mwezi mmoja, aliweza kunielezea vitabu vitatu alivyomaliza.


‎Mistari, funzo, mfano, hadi methali alizikumbuka kama ni mistari ya nyimbo.


‎Leo anaitwa “Mwalimu Musa” mtaani kwake.


‎Na kazi yake ni kufundisha wengine kusoma na kukumbuka.


‎Sasa ni zamu yako.


‎Usiendelee kupoteza muda kusoma bila faida.


‎Tumia mbinu hizi.


‎Zimejaribiwa, zimeaminika.


‎Zinakufanya usome kwa raha, na kukumbuka kama kompyuta yenye RAM kubwa.


‎Kama umefika hapa…


‎Basi moyo wako una kiu ya mabadiliko.


‎Na hakika, huo ndio mwanzo wa akili mpya.



‎Uko tayari kukikumbuka kila kitabu utakachosoma?


‎Sema: “Leo ndo mwisho wa kusoma bila kuelewa!”


‎Kama Bado Hujajiunga na Group La Usomaji Wa Vitabu,


‎Piga Simu 0750376891.


‎Karibu.

‎Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?