‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

 


‎Mpendwa Rafiki,

‎Tatizo ni moja tu: Unataka kufanikiwa.

‎ Unataka kujenga biashara. 

‎Unataka kuvutia wateja bila kuwa kero.

‎ Unataka maisha bora, lakini hujui uanzie wapi.

‎Unasikia watu wanatoka mbali kimaisha kwa kutumia maarifa, lakini wewe kila ukijaribu hakuna kinachotiki.

‎Na najua kabisa… si kwamba huna akili.

‎ Si kwamba huna bidii. La hasha!

‎Tatizo ni moja: haujapewa ramani.

‎ Haujapewa mfumo. 

‎Haujajifunza maarifa sahihi.

‎Kuna jambo linakuumiza kimya kimya…

‎Watu unaowaona wanaendelea wengi wao sio wa ajabu sana.

‎Wana siri moja tu: maarifa ya ndani.

‎Maarifa ya vitabuni. 

‎Maarifa ambayo hayafundishwi mashuleni.

‎Wanaelewa “mbinu za kuuza”, wanaijua “copywriting”, wanaelewa “psychology ya mteja”,

‎...na wanajua jinsi ya kuanzisha biashara bila mtaji mkubwa.

‎Wewe pia unaweza kujifunza.

‎Wewe pia unaweza kugeuza akili yako kuwa hela.

‎Lakini lazima ukubali ukweli mmoja:

‎ mafanikio hayaji kwa kubahatisha.

‎ Yanahitaji kujifunza.

‎Sasa hebu nikufundishe kitu kimoja…

‎Kuna vitu vitatu ambavyo ukiweza, maisha yanabadilika:

‎1. Kujifunza kupitia vitabu bora vya maarifa na ujasiriamali.

‎2. Kuandika maneno yanayouza (copywriting).

‎3. Kujenga mfumo wa kuvutia wateja bila kuwa kero.

‎Hizi ndio nguzo tatu za mafanikio ya mtaani.

‎Zinajengwa kwa kusoma vitabu sahihi, kufuatilia blog za maarifa kama Nguvu ya Vitabu, na kutenda kile unachojifunza.

‎Na ukishazielewa hakuna atakayekuzuia tena.

‎Sasa Sikiliza Solusheni Yako Iko Hapa:

‎Mimi ni Mkufunzi Ramadhan Jamaa wa Vitabu

‎Nimeanzisha hii blog ya Nguvu ya Vitabu kwa sababu moja tu:

‎Kukupa maarifa halisi ya mtaani.

‎Maarifa ya kukuinua, kukuandaa, na kukusaidia kuvutia wateja, kuuza vizuri, kuanza biashara, na kuandika maneno yanayouza bila presha.

‎Kama wewe ni kijana wa mtaani mwenye ndoto kubwa, au unataka kujua:

‎Jinsi ya kutumia vitabu kubadilisha maisha yako.

‎Jinsi ya kujifunza copywriting.

‎Jinsi ya kupata wateja bila kuwa kero.

‎Jinsi ya kuanzisha biashara bila mtaji mkubwa.

‎Hii ni blog yako. 

‎Hapa ni nyumbani kwako.

‎Sikiliza Hadithi Yangu Kidogo…

‎Miaka michache iliyopita, nilikuwa kama wewe.

‎Nimesoma sana, nimehangaika, lakini maisha hayakuwa yakibadilika.

‎Mpaka siku moja nikachukua kitabu cha kwanza cha “copywriting.”

‎Nikaelewa nguvu ya maneno. 

‎Nikaelewa jinsi wateja wanavyofikiri.

‎Nikaelewa mbinu za kujiuza bila kuombaomba.

‎Tangu hapo maisha yangu yakabadilika.

‎Leo hii, najifunza kila siku na ninashirikisha haya maarifa kupitia hii blog, semina, na kozi.

‎Na sasa nataka na wewe uanze safari yako.

‎Kama Upo Tayari Kuinuka…

‎Karibu sana kwenye Nguvu ya Vitabu

‎Hapa ndipo tunapojifunza kutumia vitabu, maarifa, na kalamu kufanikisha maisha ya kweli.

‎ Kama unataka kuandika maneno yanayouza...

‎Kama unataka kuvutia wateja...

‎Kama unataka kujifunza kupitia vitabu vya mabadiliko…

‎Karibu sana. 

‎Karibu Nguvu ya Vitabu.

‎Mkufunzi Ramadhan 

‎0750376891.

Jisajili Hapa Upate Vitabu 10

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?