‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu....


Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen?

‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?*

‎Basi sikia hii...

‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia.

‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion.

‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea.

‎Lakini...

‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku.

‎Unaitwa: Hero’s Journey.

‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa.

‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda.

‎Kama Simba kwenye Lion King.

‎Kama Neo kwenye Matrix.

‎Kama wewe kwenye maisha yako.

‎Sasa tatizo ni hili...

‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia.

‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni.

‎Wanakosa story.

‎Na bila story,hakuna connection.

‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what?

‎Wateja wanataka kujihisi wao ni mashujaa kwenye maisha yao.

‎Na kama hujawafanyia hivyo…

‎Utakula rejection mpaka uanze kujishuku.

‎Usijidanganye kuwa unahitaji maneno mengi, au Kiingereza cha kuvunja shingo.

‎Hii siyo habari ya vocabulary.

‎Ni habari ya mfumo.

‎Na huu mfumo ni silaha ya mawasiliano yenye uzito.

‎Hero’s Journey inatoka kwa Joseph Campbell.

‎Ni chombo kilichotumika kuunda filamu karibu zote kubwa duniani.

‎Wengine wanajaribu kuuza kwa ‘features na benefits.’

‎Lakini watu hawanunui features.

‎Wanunua safari ya kihisia.

‎Sasa, chukua karatasi na kalamu.

‎Andika hadithi ya mteja wako kama shujaa.

‎Hii ndiyo ramani ya Hero’s Journey (kwa lugha ya mtaa):

‎1. 👉 Anayeanza safari (Mteja wa kawaida, ana shida)

‎2. 👉 Anaona ishara (Anasikia kuhusu suluhisho lako)

‎3. 👉 Anasita (Anaogopa kujaribu, haelewi kama itawezekana)

‎4. 👉 Anakutana na kocha/mshauri (Wewe)

‎5. 👉 Anaamua kujaribu (Ananunua, anaanza kutumia)

‎6. 👉 Anapambana na vikwazo

‎7. 👉 Anakaribia kushindwa

‎8. 👉 Anasimama tena

‎9. 👉 Anashinda vita

‎10. 👉 Anarudi kama shujaa mpya (Amebadilika. Ana furaha. Ana matokeo.)

‎Ukijua kutumia hii formula unaweza kuuza kitu chochote.

‎Ngoja nikupe mfano halisi.

‎Kuna kijana mmoja anaitwa John.

‎Alikuwa hana chochote. 

‎Maskini wa kutupa.

‎Alikuwa anaishi kwa bibi yake, hana ajira, hana kipato.

‎Lakini alianza kusoma kitabu cha Nguvu Ya Buku.

‎Alianza kuweka buku tu kila siku.

‎Alianza na mtaji wa elfu tano tu kuuza maandazi.

‎Alipambana. Alikataliwa. Alichekwa.

‎Lakini hakuacha.

‎Akasoma tena. Akarekebisha. Akakutana na changamoto, lakini hakuacha.

‎Leo hii, ana duka lake. Ana wasaidizi. Ana amani kichwani.

‎Kwa sababu ya hatua ya shujaa aliyochukua.

‎Yaani mtu wa kawaida, amegeuka kuwa shujaa wa familia yake.

‎Hadithi zinauza kwa sababu watu wanajiona ndani yake.

‎Wanaona maumivu yao.

‎Wanaona tumaini.

‎Wanaona matokeo.

‎Ukijua kutumia Hero’s Journey, utaandika matangazo yanayogusa roho.

‎Utaandika post ambazo zina comments “Bro umeandika kuhusu mimi kabisa!”

‎Utaandika hadithi ambazo zinawasha moto wa kununua.

‎🔥 Basi ni muda wako sasa kuwa mwandishi wa hadithi za mashujaa.

‎👉 Wauzie watu safari, si bidhaa.

‎👉 Waonyeshe kuwa wewe ni mwongoza safari, si muuza tu.

‎Na ukitaka kujifunza jinsi ya kutumia Hero’s Journey kwenye biashara yako, 

‎Meseji moja tu inatosha!

‎Tuma Neno *Hadithi* Kwenda 0750376891.

‎Karibu.

‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir.

‎0750376891.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?