‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎ ‎Jinsi Ya Kuwashinda Washindani Bila Kuwataja Bila Vita, Bila Kelele.

 ‎*Wanazidi Kujitangaza, Wewe Watangulie Kimya Kimya*

‎Kakaa/Dadaa Yangu....

‎Unajua shida kubwa ya watu wengi?

‎Ni kufikiria ushindani ni vita.

‎Kila mtu anataka kupiga kelele, kutaja majina, kushusha wengine ili aonekane juu.

‎Lakini ukweli ni huu...

‎Watu hawapendi kelele.

‎Wanapenda thamani. Wanapenda kuaminika.

‎Na mtaa hausahau ukitoa kitu cha maana, kimya kimya.

‎Unataka ushinde sokoni?

‎Usipige kelele.

‎Toa tofauti.

‎Lakini sasa ona...

‎Wao kila siku wanapost.

‎Wanapiga picha na wateja.

‎Wanapiga video za “success.”

‎Wanasema wao ndio namba moja.

‎Na wewe unaanza kuwaza:

‎"Nikikaa kimya, nani atanijua?"

‎"Wateja watawafuata wao, si mimi?"

‎Mbaya zaidi, wengine wanaanza kukudharau.

‎Wanakuuliza, “We bado upo?”

‎Inaumaaa…

‎Sasa sikiliza kaka/dada...

‎Kelele hazijengi heshima.

‎Kelele hazijengi chapa.

‎Na kelele hazileti pesa ya kweli.

‎Ukweli ni huu:

‎Mteja hataki kujua nani mkubwa zaidi.

‎Anataka kujua ni nani atamsaidia haraka na kwa uhakika.

‎Soko lina akili.

‎Wateja wanaona.

‎Ukiwa mnyoofu, mwenye thamani watafuata.

‎Bila kushindana. Bila kutaja yeyote.

‎Hii ndo njia ya kweli ya kuwashinda washindani bila kuwataja:

‎Weka nguvu kwenye bidhaa yako.

‎Weka roho kwenye huduma yako.

‎Weka moyo kwenye mawasiliano yako.

‎Toa thamani kiasi kwamba wateja wao waanze kuwaambia:

‎*Mbona yule mwingine yuko tofauti?*

‎Usihubiri.

‎Usisingizie.

‎Toa kitu hadi washindani waanze kujiuliza:

‎*Huyu anafanya nini hadi watu wamfuate hivi kimya?*

‎Namkumbuka jamaa mmoja Mbagala.

‎Alikuwa na duka la nguo.

‎Kila mtu mtaani alikuwa anampita.

‎Maana hakupiga promo, hakusema chochote online.

‎Lakini jamaa alikuwa na staili yake:

‎Kila mteja aliyekuja, alihudumiwa kama mfalme.

‎Alipendezesha duka lake kimya kimya.

‎Akajua jina la kila mteja wake.

‎Akajua nguo gani zinampendezea nani.

‎Leo hii...

‎Washindani wake wanampost.

‎Wanamsema bila kumtaja.

‎Maana wateja wao wanawaacha na kukimbilia kwake.

‎Siri yake ni moja:

‎Alijua kupika ladha isiyohitaji mbwembwe.

‎Chukua Hili Kama Funzo:

‎Wanaopiga kelele, huisha kelele zikiisha.

‎Wanaotoa thamani, hubaki mioyoni.

‎Toa kitu mpaka kimya chako kiishike mitaa.

‎Shinda bila kubishana.

‎Washinde kwa kazi, sio kwa mdomo.

‎Anyway, kama unataka huduma ya usimamizi wa karibu,

‎Tuma meseji *NATAKA HUDUMA YA UKOCHA*

‎Kwenda 0750376891.

‎Imetoka kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?