Hupendi Kusoma Vitabu? Hizi Njia 5 Zitakubadilisha Bila Kujua!....
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Hebu niambie kaka/dada…
Ukitaja vitabu unahisi usingizi unakukamata?
Unajikuta unasema,
“Aaah mi si mtu wa vitabu bana, sina muda wala mood!”
Sawa.
Lakini je… umewahi kujiuliza,
Hii tabia ya kukwepa vitabu inakuumiza wapi?
Leo, nitaongea na moyo wako.
Sio kwa kukuhukumu.
Bali kwa kukupa mwanga wa kubadili maisha… bila stress.
Tatizo si wewe.
Tatizo ni mfumo ulivyokufundisha kusoma kama adhabu.
Ulipokuwa shule,
uliambiwa usome ili ufaulu mitihani.
Sio ili ufanikiwe kwenye maisha.
Hakuna aliyekuambia,
*Soma ili ujue namna ya kujiongezea kipato.*
*Soma ili ujue kujitetea kisheria.*
*Soma ili usilaghaiwe.*
Ndio maana sasa huoni maana ya kusoma.
Unahisi ni mambo ya watoto wa chuo tu.
Lakini ukweli ni huu:
Watu wote waliofanikiwa wanapata maarifa kupitia vitabu.
Ukitaka kujifunza siri ya pesa ipo kwenye kitabu.
Ukitaka kubadilisha mindset ipo kwenye kitabu.
Ukitaka kujua mbinu za biashara – ipo kwenye kitabu.
Na wewe bado unasema:
“Siwezi kusoma bana!”
Wakati huo huo, maisha yanakusukuma kila kona.
Umechoka na hali uliyonayo…
Lakini suluhisho linakutazama ukurasa wa kwanza tu.
Ukipita, unapata nuru.
Sasa sikiliza vizuri…
Sio lazima uwe msomi kuanza kusoma.
Sio lazima uanze na vitabu vikubwa kama Biblia.
Na wala huhitaji saa nzima.
Dakika 10 tu kwa siku zinatosha.
Na kama bado huna muda —
Una muda wa WhatsApp, TikTok, na Instagram.
Kwa hiyo muda upo, ni mindset tu haijawa tayari.
Halafu usianze na vitabu vya kuchosha.
Anza na kitu unachokipenda:
Biashara, mapenzi, mafanikio, pesa au hata stori.
Hebu chukua hizi njia 5 rahisi za kuanza kusoma hata kama huipendi:
1. Chagua vitabu vinavyokuhusu.
Usianze na “Thinking Fast and Slow.”
Anza na “Nguvu Ya Buku” au “Hadithi Za Mafanikio.”
2. Weka lengo dogo sana.
Usiseme "nitamaliza sura moja."
Sema, “Nitasoma paragraph moja tu leo.”
Ukianza hutaacha!
3. Soma muda ule ambao una amani.
Asubuhi kabla ya WhatsApp au usiku kabla ya kulala.
4. Tumia audiobook.
Unaweza kusikiliza vitabu ukiwa jikoni, gym au kwenye basi.
5. Shirikiana na mtu.
Pata mtu wa kukukumbusha au kusoma pamoja.
Hata mjadala wa mistari mitatu unaweza kukubadilisha.
Nakumbuka jamaa mmoja maeneo ya Temeke anaitwa Juma.
Alikuwa anasema:
“Mi sijawahi kupenda kitabu hata kidogo.”
Siku moja alikuta kazini kwao wanasoma kitabu fulani “Nguvu Ya Vitabu.”
Akajitahidi kusoma ukurasa wa kwanza.
Akashangaa kumbe kuna stori za mtaani mle ndani.
Akajikuta anamaliza sura tatu kwa siku moja!
Leo hii, Juma ana duka lake mwenyewe.
Anaandika bei na matangazo ya biashara yake kwa maneno ya kuvutia.
Na anasema:
“Kusoma kulinipa akili ya pesa ambayo shule haikunipa!”
Mwisho Kabisa?
Kama Juma aliweza, na wewe unaweza.
Anza kidogo, rudia mara nyingi,
Utaingia kwenye sayari mpya ya maarifa na mafanikio.
Usisubiri mpaka maisha yakulazimishe usome.
Anza leo, hata na mstari mmoja tu.
Anyway, kama unataka vitabu vizuri,
Piga Simu Kwenda 0750376891.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
0750376891
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni