Hupendi Kusoma Vitabu? Hii Ndiyo Njia Rahisi Ya Kuanza Kusoma Na Kufanikiwa Maishani!
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Jinsi Ya Kuanza Kusoma Vitabu Hata Kama Hupendi Kusoma.
Rafiki Yangu Mpendwa,
Kuna Jamaa mmoja aliwahi kuniambia kitu kilichonifanya nisahau hata njaa.
Akasema:
Mimi sihitaji kusoma vitabu. Si vipo YouTube na TikTok?
Mwaka mmoja baadaye...
Simu yake haikuwa na kifurushi.
Alichoka kuomba miamala ya 200 kwa mama wa kiosk.
Na maisha yake yalikuwa pale pale.
Mwishowe akanitext:
Bwana, tafadhali nipe jina la kile kitabu ulichonitumia. Naona sasa nahitaji kusoma…
Katika makala hii, utakutana na njia rahisi kabisa ya kuanza kusoma vitabu hata kama huwa hupendi kabisa kusoma.
Sitakuambia usome kurasa 100 kwa siku, hapana.
Nitakufundisha njia ya kuanza polepole, kwa ustadi, bila kuumiza kichwa.
Na zaidi ya yote, nitakueleza kwanini watu waliokuwa kama wewe sasa ni mamilionea.
Hebu vuta picha hii:
Unaamka asubuhi ukiwa na hamasa ya maisha.
Umejaa maarifa.
Umejua jinsi ya kutengeneza pesa.
Unajua kuzungumza vizuri mbele ya watu.
Unapendwa na watu kwa sababu ya hekima zako.
Na yote haya, si kwa sababu ulienda chuo .
Bali kwa sababu ya vitabu vitatu ulivyomaliza mwaka huu.
Mmoja ya vijana waliokuwa hawapendi kusoma, leo ni mmiliki wa biashara 3.
Alianza kwa kusoma kurasa 2 tu kwa siku.
Leo ananukuliwa kwenye redio, anafundisha wengine.
Mwingine alianza kusoma akiwa anauza chips.
Leo anamiliki duka la vitabu.
Na mshangao?
Wote walichukia kusoma mwanzoni… kama wewe.
Sasa, ngoja nikuonyeshe njia rahisi ya kuanza kusoma vitabu bila kuboreka:
✅ Usianze na vitabu vigumu.
Anza na kitabu ambacho kina hadithi. Kinachoburudisha. Kinachoeleweka haraka.
✅ Soma dakika 5 tu kwa siku.
Usijiambie *lazima nimalize sura.* Weka muda sio malengo ya kurasa.
✅ Soma mahali tulivu.
Usisome ukiwa kwenye foleni ya daladala au ukiangalia TV.
✅ Andika maneno matatu muhimu uliyojifunza.
Hii hukufanya kukumbuka zaidi na kuona thamani ya ulichosoma.
✅ Pata rafiki wa kusoma nae.
Mchangie alichojifunza. Jifunze kutoka kwake pia.
Ukweli ni huu:
Ukisubiri hadi siku utapenda kusoma haitafika.
Mafanikio hayaji kwa kubahatisha.
Yanaanza kwa maamuzi madogo.
Na uamuzi mmoja muhimu zaidi leo ni kuanza kusoma hata kurasa mbili.
Chukua kitabu kimoja leo.
Anza leo.
Sio kesho.
Sio wiki ijayo.
Leo.
Ukiendelea kukwepa vitabu, utabaki ukisubiria mafanikio ya watu wengine.
Lakini ukikubali kusoma, hata kidogo, utarusha maisha yako kiwango kingine.
Chagua leo:
Soma au endelea kusota.
Uamuzi ni wako.
Lakini kumbuka: kusoma ni njia fupi ya kufika mbali.
Anyway, Kama unataka vitabu vizuri,
Tuwasiliane Kwa Namba 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali.
Mkufunzi Ramadhan Amir.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni