‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

Hii Ndiyo Tofauti Ya COPYWRITING Na Content WRITING Wanaokuficha! 💥


‎Unajua nini?

‎Watu wengi wanajifanya waandishi,

‎Lakini wanachanganya Copywriting na Content Writing kama maji na mafuta!

‎Ni kama kuchanganya kuchoma chipsi na kufua nguo…

‎Vyote ni kazi, lakini si sawa hata kidogo!

‎Leo nakufungua macho.

‎Utaelewa tofauti kubwa sana kati ya Copywriting na Content Writing.

‎Ukimaliza kusoma hii makala, utajua ni ipi inalipa, ipi ni sanaa ya kuuza,

‎na ipi inaweza kukutoa kapa kama huitumii vizuri.

‎Fikiria upo na laptop yako,

‎Unaandika sentensi chache tu…

‎Baada ya dakika chache, mtu anakutumia pesa.

‎Copy zako zinauza bidhaa.

‎Waandishi wakubwa wa Copywriting wanalipwa hadi MILIONI kwa barua moja tu!

‎Wanaandika post moja, inauza bidhaa elfu moja.

‎Sasa waza tena…

‎Unatumia muda mwingi kuandika content,

‎Una likes, una comments, lakini hakuna mtu anayebonyeza "nunua sasa".

‎Ni kama kupiga kelele kwenye jangwa.

‎Hebu muangalie Joseph Sugarman, mmoja wa magwiji wa Copywriting.

‎Alikuwa akiandika matangazo ya kurasa 2,

‎na watu walikuwa wananunua bidhaa hata kabla hawajaiona.

‎Na hapa Bongo, kuna vijana wanaandika copies za WhatsApp tu,

‎wanafanya mauzo ya zaidi ya milioni 5 kwa mwezi.

‎Wanatumia maneno yenye "uchawi wa kuuza" hiyo ndiyo nguvu ya copywriting.

‎COPYWRITING NI NINI?

‎Ni kuandika kwa lengo la KUUZA.

‎Unapotaka mtu achukue hatua anunue, ajisajili, abonyeze, apige simu — hiyo ni Copywriting.

‎CONTENT WRITING NI NINI?

‎Ni kuandika kwa lengo la KUELEWESHA au KUBURUDISHA.

‎Inajenga mahusiano, inatoa elimu, lakini mara nyingi haichochei mauzo ya haraka.

‎Tofauti kubwa ni hii:

‎Copywriting ni SHAMBULIO inachochea hatua.

‎Content Writing ni MAZUNGUMZO — inalea uhusiano.

‎Mfano:

‎"Habari kuhusu faida za aloe vera" Content Writing.

‎"Punguza makunyanzi kwa siku 7 kwa kutumia aloe vera hii mpya Nunua Sasa!" — Copywriting.

‎ Sasa Fanya Hivi Kabla Wengine Hawajakuacha Nyuma

‎Kama unataka kuuza sana,

‎Kama unataka maneno yako yawe na nguvu ya kuchochea watu kuchukua hatua,

‎Basi jifunze COPYWRITING sasa hivi.

‎Usikose hii fursa.

‎Usiendelee kuandika content ya bure wakati unaweza kupata mamilioni kwa maneno machache tu.

‎🔥 Muda wa kubahatisha umeisha.

‎🔥 Weka mkazo kwenye maneno yanayouza.

‎🔥 Toka kwenye kundi la "waandishi wa maudhui"

‎na ingia kwenye ligi ya "waandishi wa pesa".

‎Kama bado hujui Copywriting,

‎Basi uko nyuma sana.

‎Na ukikaa kimya leo,

‎Kesho utakuta wateja wako wote wamepotezwa na yule jamaa anayejua nguvu ya maneno.

‎Tafuta kozi. Tafuta mwalimu. Tafuta mwelekeo.

‎👉 Kumbuka: Maneno Yanaweza Kukuingizia Pesa au Kukunyima Pesa.

‎💡 Unahitaji mafunzo ya Copywriting? Niachie jina lako hapa chini. 

‎Naweza kukusaidia kabla wengine hawajaja kupita na kukuwacha mbali. 🏃‍♂️

‎Tuma JINA Lako Kwenda 0750376891.

‎Karibu.

‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?