Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Tafsiri Kwa Lugha Rahisi Ya Kitabu Cha THINK AND GROW RICH.

 ‎Tafsiri Kwa Lugha Rahisi Ya Kitabu Cha THINK AND GROW RICH.


‎Usisome Kama Hutaki Kujua Siri Ya Matajiri.

‎Kakaa/Dadaa Yangu....

‎Kuna watu wamefanya kazi miaka 20… lakini bado wako pale pale.
‎Kuna watu wameenda shule, wana vyeti kibao… lakini maisha yao ni ya kusukuma siku tu.

‎Unaona kabisa mtu ana akili, ana bidii… lakini hana kitu.
‎Kwanini?

‎Kwa sababu akili peke yake haitoshi.
‎Bidii bila mwelekeo ni kama kukimbia gizani.
‎Na ndicho kitabu Think and Grow Rich kinakuambia… lakini kwa lugha ya maprofesa.

‎Leo nakuletea tafsiri ya mtaani.
‎Lugha rahisi.
‎Ile ya kueleweka hadi na mama ntilie.


‎Umewahi kujisikia kuchoka hata kabla hujaamka?
‎Ushawahi kujikuta unawaza, “Kama pesa ni mbaya, mbona sina hata kidogo?”
‎Unapigwa na stress kila mwisho wa mwezi.

‎Mshahara ukiingia, unatoka kabla haujafika kwenye simu.

‎Halafu unakutana na post ya mtu anasema:

‎“Niliwahi kusoma kitabu cha Think and Grow Rich, maisha yangu yakabadilika.”
‎Unasema “Duh! Labda kweli kuna siri humo.”
‎Lakini ukiingiza pua ndani ya kitabu, lugha yenyewe ni kama ya kozi ya udaktari.
‎Unafungia kabatini.

‎Lakini kumbe, ndani ya Think and Grow Rich, kuna vitu rahisi tu.
‎Hazihitaji PhD.
‎Hazihitaji connections.

‎Unahitaji kitu kimoja tu:
‎MAAMUZI.

‎Ndiyo.
‎Siri ya kwanza ya utajiri ni hii:

‎Taka kwa dhati, tamani kwa nguvu, amua kwa moyo wote.
‎Sio kusema tu, “Ningependa kuwa tajiri.”
‎Ni kusema, “Sitakubali kubaki maskini.”
‎Hapo ndipo kila kitu huanza.

‎Na usidanganywe:
‎Hakuna mtu aliyekuwa tajiri bila kuamua kuwa tajiri.
‎Hakuna aliyeamka tu asubuhi na kukuta account ina milioni 10 bila kufanya kitu.

‎Kwa hiyo, suluhisho ni hili:
‎Soma kitabu cha Think and Grow Rich kwa mtazamo wa mtaani.
‎Chukua funzo moja, liweke kwenye maisha yako.

‎Mfano: Kuna somo linaitwa “Mastermind” – maana yake ni hii:
‎Tafuta watu wachache wenye akili, wanaokuamini, halafu unda timu ya mafanikio.

‎Au somo la “Auto-Suggestion”

‎Ambia ubongo wako kila siku: Mimi ni tajiri. Naelekea kwenye mafanikio.
‎Unavyosema, ubongo unaanza kutengeneza njia.

‎Ni kama kuchora ramani ya mafanikio ndani ya kichwa chako.

‎Kuna mshikaji wangu mmoja anaitwa Kito.
‎Kito alikuwa fundi simu mitaani.

‎Mapato? Kawaida sana.

‎Siku moja nikampa summary ya Think and Grow Rich.

‎Nikamuambia, “Kaka, badilisha vile unavyowaza. Amini unaweza kuwa zaidi ya fundi.”

‎Alichukua somo moja “Specialized Knowledge.”
‎Akaanza kusoma zaidi kuhusu simu, akaingia YouTube, akajifunza software.

‎Leo Kito ni consultant wa maduka ya simu manne.

‎Anaingiza zaidi ya laki tano kwa wiki.
‎Na bado hajafika alipotaka.

‎Alianza na kitu kimoja: IMANI NA MAAMUZI.

‎Think and Grow Rich sio tu kitabu.
‎Ni mabadiliko ya maisha.
‎Lakini kama huwezi kukisoma chenyewe, tuliza kichwa.

‎Nitakuletea makala nyingine zaidi – za mtaani, zenye kueleweka, zenye kubadilisha maisha.
‎Usilale kabla hujapiga hatua moja mbele leo.

‎Unahitaji utajiri?
‎Basi anza kufikiri kama tajiri.

‎Kama bado hujapata tafsiri ya hiki kitabu,

‎Tuma Meseji "NIPE TAFSIRI YA KITABU CHA THINK AND GROW RICH"

‎Kwenda 0750376891.

‎Hii Makala Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection