Kakaa/Dadaa...
Watu wengi wananunua vitabu kwa hamasa kubwa.
Wanapiga picha na kuweka Instagram.
Na kuandika "nimekivuta hiki!”
Lakini baada ya kurasa tano... wameishia hapo.
Wiki mbili baadaye, kitabu kiko kabatini, kinakusanya vumbi.
Wewe mwenyewe umewahi kuanza kusoma kitabu ukakimaliza kweli?
Usijidai. Tuseme ukweli.
Na kama umewahi, je ni vitabu vingapi?
Watu hawamalizi vitabu.
Wengi Sana.
Hata wale wanaojifanya "book lovers" mitandaoni.
Unajua shida ni nini....
Unakosa maarifa muhimu.
Unajinyima fursa ya kubadilika.
Uko pale pale kimaisha.
Wenzako wanaendelea, wanachukua hatua kwa sababu wamesoma na wakatekeleza.
Wewe bado uko kwenye ukurasa wa 7, unajishawishi, “nitamalizia weekend.”
Weekend ikifika?
Unapiga mfululizo wa series 8 kwa siku moja.
Na bado unaendelea kujifariji na kusema huna muda wa kusoma!
Sasa ngoja nikutobolee siri…
Tatizo si wewe.
Tatizo si kwamba huna nidhamu.
Tatizo si kwamba huna muda.
Tatizo ni mfumo wa usomaji unaoutumia.
Unajilazimisha usome kila ukurasa kama unasoma mtihani.
Unadhani lazima usome kuanzia mwanzo mpaka mwisho.
Unadhani kusoma ni kama kula ugali wa jioni mpaka uumalize.
Wrong kabisa.
Hivyo ndivyo watu wengi wanavyoamini na wanabaki kushindwa.
Sasa hivi, hii hapa ndiyo dawa ya huu ugonjwa.
Badilisha mtazamo wako wa kusoma vitabu.
Soma kama vile unatafuta dhahabu kwenye mchanga.
Usilazimishe kusoma kila ukurasa.
Chukua kilicho cha muhimu.
Ruka sehemu zisizokusaidia sasa hivi.
Anza katikati kama huko ndiko kuna jawabu lako.
Soma kwa dakika 10 tu kila siku.
Dakika 10 tu bwana!
Na kama kitabu ni kizito sikiliza audiobook ukiwa safarini.
Usiwe na presha ya kumaliza, kuwa na njaa ya kuelewa.
Hapo sasa, utaanza kuona mabadiliko.
Kuna mdada mmoja anaitwa Jamila.
Alikuwa ananunua vitabu kwa hamu.
Akaweka shelf kali kabisa sebuleni.
Lakini hakuna hata kimoja alichomaliza.
Mpaka siku moja nikamfundisha njia hii ya "kusoma kama mtafuta dhahabu."
Akaanza kuchukua vipande muhimu, kuandika notes, kurudia sehemu alizopenda.
Leo hii, ananiambia:
“Bro, nimetoka mbali. Kitabu kimoja sasa kinanibadilisha maisha.”
Na unajua nini?
Jamila sasa anaandika kitabu chake.
Yaani yule yule aliyekuwa hawezi kumaliza sura ya pili!
Sio lazima umalize kila kitabu.
Lakini ni lazima uchukue maarifa ndani yake.
Badilika.
Soma kwa akili, si kwa mazoea.
Elimu haitoki kwenye kurasa 300 inatoka kwenye mstari mmoja tu, unaobadilisha maisha yako.
Ukishamaliza kusoma haya, usiweke tu moyoni.
Chukua hatua.
Rudi kabatini, vuta kile kitabu ulichokiacha.
Tafuta dhahabu ndani yake.
Usisome ili kumaliza soma ili kubadilika.
Kama Bado Hujajiunga Na Wenzako Kwenye Kundi La Usomaji Wa Vitabu.
Tuma Meseji *NATAKA KUNDI LA VITABU*
Kwenda 0750376891.
Karibu.
Mkufunzi Ramadhan Amir.
Maoni
Chapisha Maoni