‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Kwanini Watu Wengi Hawapendi Kusoma Na Suluhisho Rahisi La Kukusaidia.


‎Kakaa/Dadaa Yangu...

‎Kuna tatizo moja kubwa sana…

‎Watu wengi hawapendi kabisa kusoma vitabu.

‎Wanaona vitabu ni mzigo.

‎Ni kama kuambiwa uanze kufua na mikono wakati kuna mashine ya kufulia.

‎Hawana muda.

‎Hawana hamasa.

‎Na wengine, hawajui hata wapi pa kuanzia.

‎Lakini sasa ngoja nikuulize wewe:

‎Ulishawahi kununua kitabu, ukakisoma kurasa mbili, ukakitelekeza juu ya meza hadi ukakisahau?

‎Ama ulikuwa na ndoto ya kujifunza mambo fulani, ukasema “acha nitafute kitabu”

‎Lakini hadi leo unatafuta tu sababu ya kuanza?

‎Kama ni ndiyo… Haupo Pekee Yako.

‎Lakini hiyo tabia… inatuumiza sana.

‎Unajua kwanini?

‎Sababu maisha hayaendi kwa kubahatisha.

‎Tunahitaji maarifa.

‎Tunahitaji kuelewa pesa.

‎Mahusiano.

‎Biashara.

‎Uongozi.

‎Maisha yenyewe.

‎Lakini kama husomi…

‎Utaendelea kuuliza maswali yale yale.

‎Kuteseka kwa mambo ambayo wengine walishayashinda miaka mingi iliyopita kwa kusoma tu.

‎Na mbaya zaidi…

‎Ukizoea kutojifunza, akili inazoea uvivu.

‎Inaanza kuchoka mapema.

‎Inakataa kubeba ndoto zako kubwa.

‎Wewe una ndoto za kuwa milionea, lakini akili yako bado iko kwenye maelfu kwa sababu haipati mazoezi.

‎Kuna watu hudhani hawapendi kusoma kwa sababu “vitabu vinachosha.”

‎Au “hawana muda.”

‎Wengine husema, “mimi si mtu wa vitabu.”

‎Akisoma tu kichwa Cha habari tayari wanapata usingizi.

‎Lakini ukweli ni huu:

‎Sio wewe unayechoka kusoma.

‎Ni mfumo wa kusoma ndio mbaya.

‎Vitabu vingi vimeandikwa kwa lugha ngumu.

‎Kama vile vililengwa kwa maprofesa.

‎Vingine vinaboa.

‎Havikugusi. Havina stori. Havina vichekesho. Havina maisha halisi.

‎Halafu hakuna mtu aliyekuonyesha namna rahisi ya kusoma bila pressure.

‎Kwa hiyo, kila ukijaribu una-drop.

‎Sio kosa lako. 

‎Ni mfumo tu mbovu.

‎Lakini sasa, hii hapa dawa rahisi kabisa:

‎Soma vitabu vilivyoandikwa kwa lugha rahisi. 

‎Lugha ya mtaani.

‎Stori nzuri.

‎Meseji kali.

‎Somo moja moja linakuingia bila hata kuumia.

‎Kuna vitabu vinafundisha kama vile marafiki wawili wameketi kijiweni.

‎Vinafurahisha.

‎Vinakugusa.

‎Vinakuelimisha.

‎Unavikuta asubuhi, kabla hujamaliza chai tayari umekishambulia nusu.

‎Pia, badala ya kulazimisha kusoma kwa saa nzima anza na dakika tano tu kila siku.

‎Wewe soma ukurasa mmoja kila asubuhi.

‎Kesho ukurasa mwingine.

‎Baada ya wiki, akili yako itaanza kuomba vitabu yenyewe.

‎Utaingia kwenye lami ya watu wachache sana… wale wanaojifunza kila siku.

‎Bado nakumbuka vizuri…

‎Nilipokuwa chuoni, nilikuwa na chumba kilichojaa vitabu.

‎Lakini vitabu hivyo vilikaa tu kwenye shelf, vikikaa kimya kama sanamu.

‎Sikuwa nasoma hata kimoja.

‎Niliona kama ni mapambo tu.

‎Mpaka siku moja, rafiki yangu alinipa kijikitabu kidogo kilichoandikwa kwa lugha ya mtaani.

‎Kilitumia stori za mitaani, changamoto za maisha halisi, na suluhisho kali.

‎Nilikisoma hadi mwisho, bila hata kushika simu.

‎Nikagundua kumbe kumbe… tatizo langu halikuwa “sikupenda kusoma”.

‎Tatizo ni kwamba nilikuwa nasoma vitabu visivyofaa.

‎Tangu siku hiyo, maisha yangu yamebadilika.

‎Sasa nasoma kila siku.

‎Najifunza kila siku.

‎Na najua…

‎Maisha yangu ya kesho yatatokana na maarifa ninayoyapanda leo.

‎Kama na wewe umekuwa hujisomei…

‎Usijichukie.

‎Usijilaumu.

‎Chukua tu hatua moja rahisi:

‎Tafuta vitabu vinavyoeleweka kirahisi.

‎Vya lugha ya mtaani.

‎Vyenye stori kali.

‎Vyenye kukufundisha bila kukuchosha.

‎Halafu, anza kidogo.

‎Ukurasa mmoja kwa siku.

‎Ndani ya miezi michache, utakuwa mtu mwingine kabisa.

‎Ukitaka mojawapo ya vitabu kama hivyo  niambie. 

‎Kwa Namba 0750376891.

‎Nitakushauri vizuri.

‎Usikubali maisha yakupite tu ilhali suluhisho lipo mezani.

‎Karibu.

‎Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?