Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Akili Kwanza Consultants - Ndoto Mpya Inayochipua Kutoka Nguvu Ya Vitabu



Muda si mrefu uliopita, nilianzisha blogu hii kwa jina “Nguvu Ya Vitabu” kwa lengo moja kuu:


Kugusa akili za watu kupitia maarifa ya vitabu.


Nilitamani kuona vijana, wafanyabiashara, na watu wa kawaida wakigundua hazina iliyofichwa ndani ya kurasa za maarifa.


Lakini sasa…


Ndani yangu inaanza kuchipua ndoto mpya, ndoto ya kupeleka maarifa haya mbali zaidi.


Ndiyo maana leo natangaza rasmi kuanzishwa kwa mpango mpya uitwao:


Akili Kwanza Consultants

Kwa Nini Jina Hili?


Nimechagua jina hili kwa sababu lina ujumbe mzito:


  • Akili Kwanza – linaweka wazi kuwa hakuna maendeleo, mafanikio, au mabadiliko bila kuanza na mabadiliko ya fikra.

  • Consultants – linaashiria kwamba tunakwenda mbali zaidi ya kutoa tu maarifa.

Tunataka kusaidia watu kubadili maisha yao kupitia ushauri, mwelekeo, na mbinu za vitendo.


Akili Kwanza Consultants Itasimamia Nini?

Taasisi hii itajikita katika:


  • Ushauri wa kimaendeleo (maisha, biashara, na maarifa)

  • Ushauri kwa vijana na wanaoanza safari ya mafanikio

  • Kuandaa mafunzo, semina na kozi fupi
  • Kutoa maarifa ya vitabu yaliyochorwa kwa lugha rahisi, ya maisha halisi

Kwa sasa, bado ni ndoto inayoanzia humu humu ndani ya blogu hii. 


Lakini ndoto yoyote kubwa huanza kwa hatua ndogo.


Kwa Nini Naitangaza Sasa?


Naifanya ndoto hii ijulikane sasa kwa sababu nataka uitazame ukuaji wangu – hatua kwa hatua.


Unapofuatilia blogu hii, utakuwa shahidi wa ndoto inavyomea.


Leo ni wazo, kesho ni ofisi, kesho kutwa ni timu, na baadae ni shirika linalogusa maelfu ya maisha.


Mwisho: Ombi na Wito Kwa Msomaji

Endelea kusoma blogu hii…


Endelea kushiriki makala hizi na wengine…
Kwa sababu wewe ndiye sehemu ya Akili Kwanza Consultants hata kabla haijajengwa rasmi.


Kumbuka:


Maendeleo ya mtu yeyote huanza pale anapoamua kuiweka akili yake mbele ya kila kitu kingine.

Karibu katika safari hii mpya.

Mkufunzi Ramadhan
Mwanzilishi wa Nguvu ya Vitabu na Akili Kwanza Consultants

0750376891

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection