Ni Jinsi Gani Naweza Kuendeleza Tabia Ya Kusoma Kila Siku?
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
🛤️ Hadithi ya Safari Yangu Ya Kusoma:
Kutoka Kutojali Mpaka Kutegemea Kitabu Kama Maji
Miaka 15 iliyopita, mimi ndiye ningeweza kutoa sababu zote kwanini "kusoma si muhimu sana."
Nilikuwa na ratiba ngumu. Kila siku nikikurupuka asubuhi, nikiingia kwenye harakati za maisha bila kusoma hata ukurasa mmoja.
Nilikuwa na vitabu kabatini lakini vilikuwa kama mapambo. Vilikuwepo kwa heshima, si kwa matumizi.
Nilijifariji kwa kusema: “Mimi ni mtu wa vitendo, si maneno.”
Lakini ndani kabisa, nilijua kuna kitu napoteza.
Siku moja, nikiwa kwenye Facebook, nikamuona kijana mmoja akisema:
“Kama huwezi kujenga tabia ya kusoma kila siku, usitarajie kujenga biashara inayodumu, akili inayotulia, au maisha yenye dira.”
Mistari hiyo ilinipiga kama radi.
Niliisikia kweli ndani yangu. Nikagundua: ndiyo sababu najichanganya, najisahau, najiumiza ni kwa sababu najikosa.
Ndipo nilipoamua: Lazima niwe mtu wa kusoma kila siku.
Mabadiliko hayaji kirahisi. Nilijaribu kusoma asubuhi nikawa nalala.
Nikajaribu usiku nikashinda nikiangalia series.
Nilihisi aibu. "Mbona siwezi kitu rahisi hivi?"
Nilitaka kuacha. Nilihisi kama labda si mimi tu.
Lakini kuna mtu aliniambia maneno haya:
“Usilazimishe kusoma saa moja. Anza na dakika tano. Lakini usikose siku.”
Hapo ndipo nilipoamua kuachana na uzito wa kusoma ‘kama msomi’
Na kuanza kusoma ‘kama mtu anayejijali.’
Siku moja, nilianza kusoma kitabu kiitwacho "Atomic Habits" kwa dakika tano tu kila usiku.
Ndani ya kitabu hicho, nilikutana na mistari hii:
“Tabia bora hujengwa kwa kuwa mtu anayejitokeza kila siku. Hata bila motisha.”
Nilihisi kama mwandishi huyo alinijua.
Akanigeukia na kuniambia: “Wewe ni tabia zako.”
Hapo ndipo niliamua:
Kila siku, kabla sijalala, nitasoma.
Kila siku, asubuhi nikinywa chai, nitagusa angalau ukurasa mmoja.
Lakini changamoto zilikuja tena.
Simu yangu kile kiumbe cha kidijitali—ilianza kunivuta kabla na baada ya kazi.
Nilijikuta nikifungua WhatsApp badala ya Kindle.
Instagram badala ya Notes.
Na hapo ndipo nilipogundua:
Siku zote nilikuwa na muda, lakini nilikuwa nimeukodisha kwa starehe ya muda mfupi.
Nikafanya maamuzi:
Nikaweka book app kwenye home screen.
Nikaweka alarm ya “Soma Dakika 5” kila siku saa 3 usiku.
Nikaandika kwenye kioo:
“Siku ikipita bila kusoma, akili yangu inakufa kwa njaa.”
Baada ya wiki 3 za kusoma kila siku hata kidogo tu...
Nilianza kujielewa zaidi.
Nilijua ni nini kinaniumiza, na nini kinaniumba.
Maneno yangu yalitulia.
Maamuzi yangu yakawa na msingi.
Na zaidi ya yote: nilianza kujiamini.
Sikuamini ni mimi niliyekuwa natoa ushauri wa kusoma kwa wengine.
Wakaanza kuniuliza: “Unasoma vitabu gani?”
Hapo ndipo nilipogundua:
Tabia ya kusoma haijengwi kwa nguvu bali kwa mpangilio.
Na mpangilio huanza na uamuzi mmoja rahisi: “Leo, nisome ukurasa 1 tu.”
Leo hii, kusoma kwangu si mazoea tu ni ibada.
Sihitaji kusukumwa.
Nasoma kila siku kama ninavyopumua.
Na nimeahidi sitasahau nilikotoka.
Nimekuwa mtu mpya. Mwandishi mpya wa maisha yangu.
Unataka Kuendeleza Tabia ya Kusoma Kila Siku?
✍️ Anza na dakika 5 tu.
📍 Soma wakati fulani maalum kila siku.
🔁 Usikose siku, hata kama ni ukurasa mmoja.
💡 Kumbuka: Habits Build You. And Books Shape Habits.
Anyway, Kama Unataka Kujifunza Zaidi Tuwasiliane Kwa Simu Namba 0750376891.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Mwandishi|Mkufunzi Wa Mauzo Yenye Mafanikio| Kocha Wa Mafanikio Ya Mauzo.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni