Usiuze Kwa Wote Wauzie Wanaokuhitaji Zaidi!...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki,
Unapojaribu kumfurahisha kila mtu, unamkosa mtu sahihi
Mtu mmoja aliniambia, “Mimi nauza kila kitu kwa kila mtu.”
Nikamuuliza, “Unapata wateja wangapi?” Akasema, “Wachache sana!”
Hapo ndipo nilimwambia ukweli mchungu:
👉 Biashara yako si kanisa la jumapili haipaswi kuwahubiria wote.
Ukiuza kwa kila mtu, unauza kwa hakuna mtu.
Unahitaji kuelewa ni nani unayemhitaji, unayemwelewa, na anayeona bidhaa zako kama suluhisho lake.
Huyo ndiye mteja sahihi.
Katika somo hili utajifunza:
Kwa nini ni hatari kuu kuuza kwa kila mtu,
Jinsi ya kuwatambua wateja sahihi kwa biashara yako,
Mbinu 5 za kuvutia na kushikilia wateja waliolengwa vizuri,
Na jinsi ya kuacha watu “wasio wa kwako” bila kuathiri biashara yako.
Fikiria biashara yako ikiwa imejaa wateja unaowapenda, wanaokuelewa, wanaolipa kwa wakati, na wanaosambaza jina lako kwa wengine.
Hutoi ofa ovyo, hutumii muda mwingi kuwashawishi kwa sababu tayari wanajua wanachokitafuta.
Unapata faida zaidi kwa kufanya kazi kidogo, una stress kidogo, na matokeo makubwa.
Hicho ndicho hutokea unapolenga watu sahihi.
Mmoja wa vijana nilimfundisha alikuwa anauza miwani mtandaoni.
Alikuwa anajitangaza ovyo: “Miwani kwa kila mtu!” Mauzo yalikuwa mabovu.
Nilimwambia abadilishe ujumbe wake:
“Miwani ya kisasa kwa vijana wa mjini wanaojali fashion.”
Akaanza kuandika post zenye mvuto wa kisasa, picha nzuri, na hadithi fupi za mitindo.
Wiki ya kwanza alipata oda 13.
Alivyolenga kundi dogo, alifanya mauzo makubwa.
Hapa Kuna Njia 5 Za Kulenga Wateja Sahihi:
1. Mtambue Mteja Wako Bora (Ideal Customer):
Uliza maswali haya:
Ana umri gani?
Anakaa wapi?
Ana matatizo gani yanayohusiana na bidhaa/huduma yako?
Ana ndoto gani? Anaogopa nini?
Mfano: Ukiuza bidhaa za ngozi, je unawalenga wanawake wa mjini wanaopenda skincare?
Usijifanye unamfurahisha kila mtu mwenye ngozi.
2. Andika Kwa Lugha Ya Mteja Sahihi:
Kama unawalenga vijana wa mjini, usiandike kama mzee wa baraza la ushauri.
Kama unawalenga wa mama wa familia, elewa maneno yao, mitazamo yao, na maisha yao ya kila siku.
Mfano:
Badala ya kusema “Mafuta haya yana virutubisho vizuri kwa ngozi,
Sema “Mama mrembo, mafuta haya yatakusaidia kuondoa madoa na kurudisha furaha ya kujiangalia kwenye kioo.”
3. Tangaza Kwenye Sehemu Sahihi:
Ukiuza vifaa vya kilimo, usitumie muda mwingi kwenye Instagram.
Nenda Facebook au vikundi vya wakulima.
Ukiuza huduma kwa freelancers au wajasiriamali, tafuta LinkedIn au WhatsApp groups za kitaalamu.
Habari njema ni kwamba zile mbili (2) za dhahabu,
Unaenda kuzipata ndani ya kitabu hiki kipya kinachoitwa*NDOANO YA KISASA*
Kupata kitabu hiki piga simu 0755376891.
Au tuma ujumbe "NDOANO YA KISASA" Kwenda 0755376891.
Kumbuka:
Siri ya mvuto wa wateja ni hii:
Usitake kumfurahisha kila mtu mfurahishe mtu wako sahihi.
Mteja sahihi anakuona, anakuelewa, anakutafuta, na anakuamini.
Anza leo kuwa mteja wa aina hiyo kwa biashara yako.
Futa ujumbe wa jumla.
Chagua mteja wako.
Jenga sauti yako.
Vutia kwa usahihi.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Mwandishi| Mkufunzi|Kocha.
0755376891.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni