Sina Muda Ni Uongo Unaouamini...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu,
Hii ni sababu Pekee Inayokuzuia Kusoma na Kubadilika.
Kama huna dakika tano za kusoma leo, huna haki ya kulalamika kesho kwamba maisha yako hayajabadilika.
Ni kauli maarufu sana miongoni mwa watu wa mtaani:
*Mimi napenda kusoma, lakini sina muda.*
Kila mara nikisikia mtu anasema hivyo, najua huyu hajawahi kuhesabu saa zake.
Hebu fikiria, unapoamka asubuhi, hadi unapolala usiku, kweli hakuna dakika tano za bure?
Hakuna muda wa kusubiri foleni kwenye daladala, benki, hakuna dakika ya kusubiri chakula kiive, hakuna muda wa dakika chache kabla ya kuingia kazini?
Ukweli ni kwamba, muda upo, ila tunauharibu kwa kufanya mambo madogo madogo.
Brian Tracy kwenye kitabu chake cha Eat That Frog First anasema:
Kama hutapanga muda wako, mtu mwingine atakupangia.
Na ndiyo maana unaona siku inakimbia, halafu unabaki na hali ile ile mwaka hadi mwaka.
Huu msemo wa sina muda ni uongo tuliojifundisha kuuamini ili kujisamehe kwa kutokuchukua hatua.
Ni kama ngao ya kujificha ili tusikabiliane na ukweli wa uvivu wetu au vipaumbele vibaya.
Bado....
Namkumbuka rafiki yangu mmoja anaitwa Hassan, fundi simu pale Kariakoo.
Ilikuwa kila nikifika ofisini kwake, simu yake iko mkononi, anajibu WhatsApp, anatazama video, au anaangalia TikTok.
Nilimuuliza siku moja:
Hassan, umewahi kusoma kitabu?
Akanijibu kwa kicheko:
Aaah kaka, sina muda wa mambo hayo.
Kazi yenyewe inanibana sana.
Nilimwambia tufanye jaribio.
Nikampa kitabu kidogo sana Cha Eat That Frog First. Nikamwambia:
Soma dakika tano tu kila siku, kabla hujaanza kufungua simu ya mteja yeyote.
Tulianza siku ya Jumatatu.
Kila asubuhi alifika kazini dakika 15 mapema, akasoma kurasa mbili au tatu.
Baada ya wiki tatu, alimaliza kitabu kizima.
Lakini kilichonishangaza zaidi si kwamba alimaliza kusoma, bali alianza kutumia mbinu za kupanga kazi alizojifunza.
Wiki chache baadaye, alinipigia simu akisema:
Kaka, sasa nafanya kazi kwa mpangilio.
Na bado napata muda wa kupumzika.
Hata wateja wameongezeka kwa sababu siwachanganyi tena na simu nyingi mezani.
Hassan hakupata muda wa kusoma aliutengeneza.
Hii ndiyo mbinu ya dakika tano iliyonisaidia mimi na watu wengi niliowafundisha:
Mbinu: “Dakika 5 za Dhahabu”
1. Amua muda maalum kila siku, Asubuhi kabla ya simu, mchana wakati wa mapumziko, au jioni kabla ya kulala.
2. Chagua kitabu kimoja tu,Usianze na vitabu vitatu mara moja, akili itachoka.
3. Weka saa yako kwa dakika 5 Simu yako ina timer, itumie.
4. Soma kwa umakini Usiruke ruke kurasa.
5. Andika mstari mmoja wa funzo, Hata kama ni sentensi moja, iandike ili ikae kichwani.
Unapofanya hivi kila siku, hutegemei “mood” ya kusoma, unategemea ratiba. Na ratiba haijali kama una muda au huna inakulazimisha kuupata.
Ukianza kutumia Dakika 5 za Dhahabu:
Unashinda kikwazo cha kuanza. Kuanza ndiyo ugumu, na dakika tano zinaondoa vizuizi.
Unajenga tabia ya kila siku, Tabia hujengwa kwa msimamo, si kwa nguvu ya ghafla.
Unamaliza vitabu bila kujisumbua.
Dakika tano x siku 365 = angalau vitabu 12 vidogo kwa mwaka.
Unapandisha kiwango cha maarifa yako Kila kitabu ni mwalimu mpya.
Unajenga nidhamu ya vipaumbele Kama unaweza kupata muda wa kusoma, unaweza kupata muda wa kufanya kitu chochote muhimu.
Leo, fanya kitu kimoja tu:
Chukua kitabu, weka saa yako dakika tano, soma, na andika kitu kimoja ulichojifunza.
Ukimaliza, tafakari: kama dakika tano zinaweza kuleta tofauti hivi, itakuwaje nikizidisha mara mbili?
Usisubiri kesho.
Kesho ni kisingizio kipya.
Karibu.
0750376891
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni