Matajiri Husoma, Wajinga Huwacheka...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu....
Kwanini Wenye Akili ya Fedha Hupenda Vitabu, na Wenye Dhihaka Huendelea Kukwama
Umeshawahi kumuona mtu anapiga hatua kubwa kimaisha, na ukajiuliza *Amewezaje?*
Au umewahi kumkejeli mtu anayewekeza muda wake kusoma vitabu badala ya *kutafuta hela*?
Kuna siri moja rahisi:
Matajiri hawakimbii vitabu, wanavikimbilia.
Wajinga huwacheka, lakini baada ya miaka michache, maisha ya watu hawa mawili huwa ni kama usiku na mchana.
Tatizo kubwa ni fikra potofu tulizolishwa:
*Kusoma ni kwa watoto wa shule pekee.*
*Ukitaka pesa, tafuta kazi, si kusoma vitabu.*
*Vitabu havikupi hela mkononi.*
Wengi huamini maarifa ya shule yanatosha, na baada ya hapo wanajifunga kimasomo.
Wakati huo, wale wenye akili ya kifedha huendelea kusoma, siyo tu vitabu vya shule, bali vitabu vya biashara, uwekezaji, uongozi, na maendeleo binafsi.
Robert Kiyosaki, katika *Rich Dad Poor Dad*, anaeleza tofauti kati ya “Baba Tajiri” na “Baba Masikini*.”
Baba Masikini aliamini elimu inamalizika baada ya shule.
Baba Tajiri aliamini kujifunza hakumaliziki—ila lilikuwa jukumu la kila mtu anayetaka uhuru wa kifedha.
Matokeo? Baba Tajiri alitumia vitabu kama ramani ya kuiendesha pesa.
Baba Masikini alibaki akitafuta mshahara kila mwezi, akipambana na gharama.
Huu ni mfano wa Hussein “Baba Juma” kutoka Magomeni.
Hussein alikuwa na kiosk kidogo cha kuuza simu na vocha.
Kila alipokuwa na muda wa ziada, alikuwa anakaa na marafiki mtaa wa pili, wakicheka wale *wanaosoma vitabu vya Fedha*”
Walimwambia, “Hizi ni hadithi tu, maisha ni kuhustle!”
Lakini jirani yake, Juma, alianza kusoma vitabu vya fedha, ikiwemo Rich Dad Poor Dad.
Kila wiki Juma alikuwa anazungumza kuhusu “mtiririko wa fedha” na “vyanzo vya mapato.”
Hussein na wenzake walimcheka.
Miaka mitatu ilipita:
Hussein bado alikuwa na kiosk, akipambana kulipa kodi.
Juma alikuwa na maduka matatu ya vifaa vya umeme, alikuwa amewekeza kwenye nyumba ndogo za kupanga, na alikuwa akisaidia vijana kupata ajira.
Hussein alijikuta akimuuliza Juma, “Bro, ulifanyaje?”
Jibu la Juma lilikuwa rahisi:
“ *Nilisoma, nikajifunza, nikatumia kile nilichosoma*. *Wewe uliniangalia na kunicheka.*
Hii hapa mbinu ya dakika 5 inayokufanya uanze “kusoma kama matajiri” badala ya kucheka kama waliobaki nyuma:
Hatua ya 1: Chagua kitabu kimoja cha maendeleo binafsi au biashara.
Usianze na orodha ndefu anza na kitabu kimoja kilichosifiwa (mfano: Rich Dad Poor Dad).
Hatua ya 2: Soma kurasa chache kila siku
Lenga kurasa 5–10 kwa siku. Dakika 5 tu zinatosha.
Hatua ya 3: Andika jambo moja la kutekeleza
Kila ukisoma, andika kitu kimoja ambacho unaweza kujaribu au kufanyia maamuzi.
Hatua ya 4: Chukua hatua hiyo kesho.
Usikae na maarifa kichwani pekee—yatumie.
Mfano: Ikiwa umejifunza kuhusu kutenga asilimia 10 ya kipato kwa akiba, anza kesho.
Hatua ya 5: Jadili ulichosoma na mtu mwingine
Mazungumzo yanasaidia kumbukumbu na kukuza mtandao wa watu wenye malengo kama yako.
Kama ukianza kusoma na kutumia vitabu kama chanzo cha maendeleo, utaona mabadiliko haya:
Mawazo mapya ya biashara na uwekezaji ambayo huwezi kuyapata kwa kukaa tu na marafiki.
Kujua lugha ya pesa: Mapato, mali, madeni, mtiririko wa fedha.
Kujiamini kufanya maamuzi ya kifedha kwa sababu una msingi wa maarifa.
Kuona fursa mapema kuliko wale wanaocheka na kupuuzia elimu ya kifedha.
Kuvutia marafiki wapya wenye malengo makubwa watu wanaokutia nguvu badala ya kukuvuta chini.
Kujenga urithi maarifa unayopata unaweza kuwafundisha watoto au ndugu zako, kuwapa mwanzo bora maishani.
Kuhama kutoka kufanyiwa maamuzi, hadi kufanya maamuzi unakuwa bosi wa maisha yako.
Leo hii, fanya uamuzi ambao wengi hawatafanya:
Chagua kitabu kimoja cha kifedha au maendeleo binafsi.
Soma kurasa chache kila siku.
Tumia angalau wazo moja unalolisoma kila wiki.
Kumbuka, kila mara unaposoma, unajenga *mtaji wa akili* ambao hakuna mtu anayeweza kukuibia.
Matajiri hujua hili; ndio maana hawakimbii vitabu, wanavikumbatia.
Usiwe yule anayekaa pembeni akicheka kuwa yule atakayesomwa hadithi yake miaka ijayo.
Soma. Jifunze. Tumia. Rudia.
Hii ndiyo njia ya kuingia kwenye ligi ya waliofanikiwa.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Karibu.
0750376891.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni