Huwa Hupendi Kusoma Vitabu? Hii Ndiyo Dawa Yako*….
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki,
Hupendi Kusoma? Subiri Uone Siri Hii.
Rafiki Yangu,
Ulishawahi kushika kitabu, na ukasoma kurasa mbili tu, ukachoka hoi bin taabani?
Kurasa mbili tu zikaonekana kama umebeba mawe ya Mtwara?
Kuna watu hawapendi kabisa kusoma.
Si kwa sababu hawana akili, wala hawajui kusoma, la!
Ni kwa sababu ubongo wao umezoea burudani rahisi kama TikTok, Instagram, video za dakika moja mpaka kitabu kinaonekana kama maumivu.
Na kumbuka, hatukuzaliwa tukiwa hatupendi kusoma.
Hiyo chuki ya vitabu ni tabia iliyojengeka kidogo kidogo.
Ulipoanza shule labda ulikuwa na shauku, lakini ulipoambiwa usome vitabu visivyo na ladha, bila mtu kukuonyesha maana yake kwenye maisha yako, ukaanza kuviona kama adui.
Halafu ukakua, ukaingia kwenye maisha ya kila siku, kazi, msongo, bili na sasa hata kurasa tano zinaonekana kama mzigo.
Lakini ukweli mchungu ni huu:
Kama huwezi kufurahia kusoma, unajinyima njia rahisi zaidi ya kujua siri za maisha.
Nikupe stori ya Baba Rashid, dereva wa bodaboda pale Sinza.
Yeye alikuwa haoni umuhimu wa kusoma.
Anasema, Mimi siyo mtu wa vitabu, mimi ni mtu wa kazi.
Vitabu vilikuwa kwake kama vipande vya karatasi visivyo na hela ndani.
Siku moja, jamaa yake akamletea kitabu kidogo Kinachoitwa *The Miracle Morning*
Alimwambia, “Soma ukurasa mmoja tu kila asubuhi, kabla hujapanda pikipiki.”
Baba Rashid akacheka, lakini akasema, *Basi ngoja nijaribu, ili tu nikurizishe vitabu havinifai.*
Wiki ya kwanza alisoma kurasa chache tu, lakini akagundua kitu:
Kadiri anavyosoma asubuhi, akili yake inakuwa fresh siku nzima.
Baada ya mwezi mmoja, alianza kufurahia.
Sasa hivi, Baba Rashid ana vitabu vitano kwenye shelfu yake na anasema, *Siku nisiposoma, najisikia kama nimekosa chai ya asubuhi.*
Sasa, kama na wewe hupendi kusoma, hapa kuna dawa ya dakika 5:
Mbinu inaitwa *Ukurasa Wa Asubuhi.*
Inasema….
Kila asubuhi, kabla hujashika simu au kuanza shughuli, chukua kitabu cha kuvutia.
Usijiwekee lengo kubwa, sema: *Nitasoma ukurasa mmoja tu.*
Baada ya siku 7, ongeza hadi kurasa 2 au 3.
Usijilazimishe kumaliza sura nzima acha sehemu ikatike pale unapofurahia, ili kesho usubiri kwa hamu kuendelea.
Hii ni Saikolojia ndogo: unapojinyima kumaliza sehemu nzuri, ubongo wako unakuwa na hamu ya kuendelea kesho.
Ukianza kufanya hivi, ndani ya mwezi mmoja utaona mabadiliko haya:
Ubongo wako utaanza kuona kusoma kama burudani, si kazi ngumu.
Utakuwa na maneno na mawazo mapya ya kutumia kila siku.
Kiwango chako cha kujiamini kitaongezeka kwa sababu unajua kitu ambacho wengi hawajui.
Utaanza kuona uhusiano kati ya vitabu na maisha halisi.
Halafu, bila hata kutambua, utakuta unasoma kurasa 10, 20… na bado unafurahia.
Usisubiri hadi *upate mood* ya kusoma mood haitakuja.
Anza kesho asubuhi.
Chukua kitabu kimoja, soma ukurasa mmoja tu kabla ya kushika simu.
Utakapofanya mara 7 mfululizo, nakuhakikishia utakuwa mtu bora sana.
Kupata Masomo Kama Haya Bure,
Tuma Meseji "NIUNGE"
Kwenda 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Mwandishi| Mkufunzi| Kocha
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni