Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Hii Ndio Shortcut ya Maisha*

 Rafiki Yangu,


Sekunde Chache Zijazo Utajifunza...


Njia Fupi ya Kuelekea Mafanikio, Bila Kupoteza Miaka Ukiangaika.


Hivii....


Umeshawahi Kujiuliza kwanini wengine wanafanikiwa haraka sana ilhali wewe bado uko pale pale?


Wakati wengi wanapoteza miaka wakijaribu njia zote, wachache wanatumia dakika chache kusoma maarifa yaliyowachukua wengine miongo mingi kuyajenga.


Changamoto kubwa ya watu wengi ni hii: wanataka matokeo ya haraka, lakini wanakataa kujifunza kutoka kwa waliotangulia.


Badala yake:


Wanajifunza kwa majaribio na makosa bila mwongozo.


Wanarudia makosa ambayo wengine tayari walishayaepuka.


Wanaona kusoma vitabu kama jambo la kuchosha na linalopoteza muda.



Kitabu Cha  *Tools of Titans cha Tim Ferriss* kinafunua siri kubwa:


Watu wanaofanikiwa hawasubiri kugundua kila kitu peke yao, wanakopi, kurekebisha, na kutumia mbinu bora za wale waliowahi kufanikisha mambo makubwa.


Tatizo ni kwamba wengi wetu tumeshtukizwa na kasumba ya *lazima nipate uzoefu wangu mwenyewe,* na kusahau kuwa kusoma ni tiketi ya kujipatia uzoefu wa wengine kwa bei nafuu sana,


...mara nyingi bila gharama yoyote zaidi ya muda wa dakika chache.


Halima ni mama wa watoto wawili kutoka Mbagala. 


Alikuwa na ndoto ya kuanzisha biashara ya kuuza bidhaa mtandaoni, lakini kila mara alikuwa akihisi amepotea. 


Alijaribu mara mbili na kufilisika mara ya kwanza kwa kuagiza bidhaa ambazo hazikuwa na soko, na mara ya pili kwa kutumia matangazo ghali yasiyo na matokeo.


Siku moja, Halima aliangukia kipande cha mahojiano cha Tim Ferriss kwenye YouTube.


 Alisikia akisema:



* *Smart people don’t reinvent the wheel they learn from people who have already built the wheel.*



Aliguswa sana.


 Akaamua kuanza na kitabu Tools of Titans.


 Alipata hadithi na mbinu kutoka kwa wafanyabiashara, wanariadha, na wavumbuzi waliopitia changamoto kubwa kuliko zake.


Ndani ya wiki tatu:


Alijifunza jinsi ya kufanya utafiti wa soko kabla ya kuagiza bidhaa.


Alijua mbinu ya matangazo yenye gharama nafuu lakini yenye kufikia wateja sahihi.


Alipata wazo la “pre-order” (kuchukua oda kabla ya kuagiza bidhaa), lililomwokoa kupoteza mtaji tena.



Miezi sita baadaye, Halima alikuwa akipata faida ya kutosha kulipia ada ya watoto wake, akisema:


*Kama ningesoma mapema, ningeokoa miaka miwili ya makosa na hasara.*


Una dakika 5 za Kuchukua Shortcut Yako ya Maisha Leo.


Hatua 1: Tambua Lengo Lako la Haraka


Ni nini unachotaka sasa? Fedha zaidi? Afya bora? Uwezo wa kuongea hadharani?



Hatua 2: Tafuta Kitabu Kinachohusiana Moja kwa Moja na Lengo Lako


Badala ya kusoma chochote tu, chagua kilicho na matokeo unayoyataka.



Hatua 3: Tafuta Hadithi au Mbinu Moja Kutoka kwa Mtaalamu


Kama ilivyo Tools of Titans, tafuta somo la mtu aliyefanikisha jambo unalotaka.



Hatua 4: Andika na Upange Kuitumia Mara Moja


Sio kusoma tu buni mpango wa kutumia hiyo mbinu kabla siku haijaisha.



Hatua 5: Rudia Kila Siku


Hata kama ni somo dogo sana, kila siku unajenga “akiba” ya maarifa yanayokupa njia fupi zaidi ya mafanikio.



Unaokoa miaka ya majaribio yasiyo na tija unajifunza kupitia uzoefu wa wengine.


Unapata suluhisho lililothibitishwa hakuna kubahatisha.


Unajenga mtazamo wa kitaalamu haraka unafikiri kama mtaalamu kabla hata hujawa mtaalamu.


Unapata motisha ya papo kwa papo kuona mtu aliyefanikisha huamsha imani yako.


Unapanua mitazamo yako unajifunza mbinu kutoka kwenye sekta na mazingira tofauti.


Unakuwa na kasi kubwa ya maendeleo unapita hatua nyingi kwa muda mfupi.


Leo, fanya jambo moja:


Tafuta kitabu kimoja kinachokupa *shortcut* kwenye ndoto yako.


Soma angalau ukurasa mmoja wa somo la mtu aliyefanikisha unachotaka.


Andika hatua moja utakayoichukua kesho kutokana na hayo.


Kumbuka, kama Tim Ferriss anavyosema:


*You are the average of the five people you associate with most, including the books you read.*



Weka kitabu hicho mikononi mwako leo, na ujifunze kutoka kwa wale waliowahi kufanikisha kile unachotamani,


Hiyo ndiyo njia fupi zaidi ya kufika kule unakotaka kufika.



Karibu.

0750376891.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection