Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Ukweli Wa Kushangaza: Mara Ya Pili Nilipokisoma… Ndipo Nilipokisoma Kwa Mara Ya Kwanza.....

‎Je, unapaswa kusoma kitabu mara moja au mara nyingi? 

‎Hadithi hii itakupa jibu la moyo....

‎Nilikuwa na orodha ndefu ya vitabu.

‎Niliamini mafanikio yangu yanategemea idadi ya vitabu nilivyomaliza.

‎Nikawa najisifu: “Nimesoma vitabu 12 mwaka huu!”

‎Lakini cha kushangaza, sikumbuki hata sura ya kwanza ya vitabu vitano.

‎Nilikuwa msomaji mwenye kasi, lakini si mwenye mabadiliko.

‎Siku moja nikakutana na nukuu:

‎Don’t just read more books.

‎ Reread the right ones.

‎Nukuu hiyo ilinichoma kama sindano ya kweli.

‎Nikajiuliza: “Ina maana nasoma sana lakini bado nipo palepale?”

‎Nilijitetea:

‎“Mbona kusoma kitabu mara moja tu inatosha? 

‎Sina muda wa kurudia! Kuna vitabu vingapi bado sijavifungua?

‎Niliona kurudia kitabu kama kurudia darasa uliokwisha kufaulu.

‎Lakini ndani kabisa, nilihisi kuna kitu kinakosekana.

‎Nikamkuta mjasiriamali mmoja aliyenukuliwa kwenye podcast:

‎.Mimi husoma vitabu vichache lakini kila mwaka narudia vitabu vitatu muhimu.

‎Kila mara nagundua hazina mpya.

‎Akanitajia kitabu alichokisoma mara tano, na jinsi kila usomaji ulivyomletea mafanikio mapya.

‎Nilitulia. Nikasema:

‎"Na mimi nitajaribu."

‎Nikachukua kitabu nilichokisoma miezi 6 iliyopita: “Atomic Habits.”

‎Nikaanza kusoma tena lakini safari hii kwa utulivu.

‎Kila ukurasa uligusa maeneo ya maisha yangu niliyokuwa sikuyazingatia hapo awali.

‎Nikagundua kwamba usomaji wa mara ya pili… ndio ulikuwa wa kwanza wa kweli.

‎Wengine walinishangaa:

‎"Umerudia tu hicho kitabu? Kwani hakuna kingine?"

‎Lakini mimi niliona tofauti.

‎Nikaanza kuandika journal.

‎Nikatekeleza hatua moja moja.

‎Nikaanza kuona mabadiliko halisi maishani.

‎Nilipoanza kutekeleza aliyosema mwandishi, nikakutana na vikwazo.

‎Nikaona ugumu wa kubadili tabia.

‎Nikashawishika kusema:  *Haya yote si rahisi kama alivyoandika.*

‎Lakini nikakumbuka:

‎*Mwandishi alishasema mazoea huhitaji uvumilivu.*

‎Niliendelea.

‎Wiki chache baadaye, maisha yangu yalibadilika:

‎📌 Nikaacha kurudia makosa yaleyale.

‎📌 Nikaweka ratiba za kweli.

‎📌 Nikaanza kuona matokeo.

‎📌 Nikaanza kuishi kile nilichokisoma.

‎Nikaanza kuhamasisha wengine:

‎"Usiwe na haraka ya kukusanya vitabu. Kusanya tabia."

‎Nikaanza kozi ya kusoma kwa kina si kwa haraka.

‎Watu wakaanza kuniambia:

‎"Kwa mara ya kwanza nimesikia mtu akisema tusome kitabu kimoja mara nyingi kuliko vitabu vingi mara moja."

‎Sasa mimi ni msomaji tofauti.

‎Ninapoona kitabu kizuri, siwezi kukiacha kwa usomaji mmoja tu.

‎Naona kina vipindi tofauti vya maisha yangu.

‎Kila usomaji mpya unaniambia kitu tofauti.

‎Sina haraka.

‎Ninapenda kina.

‎Nimekuja kukwambia hivi rafiki:

‎Kitabu kizuri si cha kusomwa mara moja ni cha kuishiwa nacho mara nyingi.

‎Kama kuna kitabu kilikugusa, kirudie tena.

‎Kila safari ya kurudia inakuletea zawadi mpya.

‎Usiwe msomaji wa haraka kuwa msomaji wa mabadiliko.

‎Kujiunga Na Wasomaji Makini Wa Vitabu,

‎Nipigie au Nitumie ujumbe kwenda 0750376891.

‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Kocha Ramadhan Amir, 

‎Mwandishi | Mkufunzi Wa Mauzo Ya MAFANIKIO | Kocha Wa MAFANIKIO Ya Mauzo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection