🔥 Story: Nilipochoka Kuishi Maisha Duni...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Safari Ya Kujiokoa Kwa Vitabu
Nakumbuka Miaka 9 iliyopita nilikuwa mtu wa "tutasonga tu."
Nilikuwa na maisha ya kawaida, kazi ya kawaida, ndoto za kawaida na hata mawazo ya kawaida.
Lakini moyoni…
Nilihisi kuna kitu nakikosa.
Nilikuwa hai, lakini si mzima.
Nilicheka, lakini ni kwa Kujilazimisha.
Niliamka kila siku, lakini bila msisimko.
Ilikuwa kama maisha yananipita tu na mimi nikiangalia kama mgeni.
Siku moja, nilikutana na rafiki mmoja wa zamani alikuwa tofauti.
Anang'ara. Anaongea kwa uthabiti. Ana maono.
Nikamwambia:
“Bro, umebadilika sana. Ulifanya nini?”
Akaniambia kwa upole,
“Niliamua kuanza kusoma vitabu sahihi. Ndipo maisha yangu yakaanza kubadilika polepole.”
Nikacheka kwa kejeli:
“Vitabu tu?”
Akaniambia,
“Ndiyo. Lakini si vitabu vyovyote. Vitabu vya kujijenga. Vitabu vya kuamka tena. Vitabu vya kujikomboa.”
Nilirudi nyumbani nikiwa na changamoto kichwani.
Mimi? Kusoma vitabu? Mimi si mtu wa vitabu.
Niliona kama hiyo ni kwa watu ‘serious.’ Mimi nilizoea TikTok, WhatsApp, Fb, Instagram, YouTube na Netflix.
Nilijidanganya:
“Mimi najua maisha kwa vitendo, si kwa kusoma.”
Lakini moyoni, nilijua nimeshikika.
Siku kadhaa baadaye, nilimpigia tena yule rafiki.
Nikamuuliza,
“Ni vitabu gani hasa ulianza navyo? Nataka tu nijaribu. kimoja tu.”
Akacheka, akasema,
“Niko tayari kukuongoza. Ila usisome kwa haraka soma kwa kuokoka.”
Akanitumia listi ya vitabu 5 vya kuanza upya:
📚 Vitabu Vya Kuanza Upya Maisha Yako:
1. “The Power of Now” – Eckhart Tolle
Unajifunza kuachilia yaliyopita na kuishi sasa. Hapa ndipo safari ya ndani huanza.
2. “Atomic Habits” – James Clear
> Unaanza kujenga maisha mapya kwa tabia ndogo ndogo kila siku.
3. “Awaken the Giant Within” – Tony Robbins
Unagundua nguvu kubwa iliyo ndani yako ambayo haijawahi kutumika.
4. “The Four Agreements” – Don Miguel Ruiz
Unajifunza kuachilia mitazamo ya jamii na kuishi kwa uhuru wa kweli wa akili.
5. “The Alchemist” – Paulo Coelho (Riwaya ya Kiroho)
Unajifunza kuwa kila mtu ana “hazina” yake safari yako ni ya kipekee.
Nilinunua vitabu viwili vya mwanzo.
Nikaamua: “Nitavisoma mpaka mwisho,
Hata kama ni ukurasa mmoja kwa siku.”
Kila ukurasa ulinifungua.
Kila sentensi ilikuwa kama dawa.
Nilianza kuona mwanga mdogo mbele ya handaki.
Wakati mwingine nilichoka. Marafiki wakanicheka:
“Eti unataka kubadilisha maisha kwa kusoma vitabu? Hahaha!”
Lakini kila nilipohisi kuvunjika moyo, ukurasa mmoja wa kitabu changu ulinikumbusha:
“Mabadiliko huanza ndani. Si kwa kelele, bali kwa utulivu.”
Nakumbuka usiku mmoja nilijikuta nikilia peke yangu.
Nikakumbuka maneno ya Tolle:
“Suffering is necessary… until you realize it’s not.”
Hapo ndipo nilipoamka kwa mara ya kwanza si kwa macho, bali kwa roho.
Miezi sita baadaye…
Nilikuwa mtu mpya.
Nilianza biashara ndogo.
Niliacha ulevi.
Nilianza kujiamini.
Watu wakaanza kuniuliza:
“Wewe umetumia dawa gani?”
Nikawaambia kwa utulivu,
“Nilianza kusoma vitabu vinavyobadilisha maisha.”
Sasa najua si lazima uzaliwe tajiri.
Si lazima uwe na bahati.
Si lazima uwe chawa.
Unachohitaji ni kuamua kuanza upya, kwa kitabu kimoja tu.
Mimi ni yuleyule kwa jina.
Lakini ndani yangu, mimi ni mtu tofauti kabisa.
Mimi ni kiongozi wa maisha yangu.
Na kila siku huanza na kurasa kadhaa za kunionyesha njia.
Na sasa nimekuja kukuambia wewe pia:
"Ukichoka kuishi maisha duni, soma vitabu visivyo vya kawaida. Ndipo utakapoishi maisha yasiyo ya kawaida."
Unataka kuanza upya maisha yako?
Usianze na pesa. Usianze na watu.
Anza na ukurasa mmoja.
Anza na kitabu kimoja.
📚 Na uanze leo.
Tuwasiliane Kwa Namba 0750376891.
Nikupe Hivo Vitabu.
Karibu.
Rafiki Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni