🧨 Maneno Ya Kuuza vs Maneno Ya Kawaida Jifunze LUGHA YA MAUZO.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu,
🛑 Acha tuanze na swali moja rahisi:
Ungependa mtu akusikie...
au akusikie na achukue hatua?
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuongea tu, na kuongea hadi mtu avue viatu akimbie kununua kitu chako.
Karibu kwenye darasa la mtaa hapa unajifunza maneno ya kuuza, si maneno ya kupoteza muda.
🔥 1. Watu Wengi Wanakosea Hapa Hawajui Kuzungumza LUGHA YA MTEJA
Wanauza kama wanaelezea.
Wanashawishi kama wanahubiri.
Wanatumia maneno ya kawaida kwenye kazi ya kuuza.
Mfano:
“Hii ni bidhaa bora sana.”
“Tuna huduma nzuri.”
“Karibu tukuhudumie.”
Yaani mtu anasikia, lakini hashtuki. Hakuna msisimko. Hakuna kichwa kumruka.
Matokeo yake? Wanapitwa tu na wanaojua kuchagua maneno sahihi.
💣 2. INAKERA! Unajua Kitu Chako Ni Kizuri, Lakini Watu HAWANUNUI!
Unajituma.
Unajua bidhaa yako ni ya maana.
Lakini ukiweka tangazo, ni kama umeandika barua ya maombi.
Ni kama vile unawaomba wanunue, badala ya kuwafanya watamani hadi wasilale.
Hapo ndipo penye uchungu.
Unalipa matangazo, unachoka kutuma meseji, unajitahidi kutoa ofa... lakini response ni ya kushangaza.
👉 Tatizo si bidhaa yako. Tatizo ni lugha unayotumia.
🧠3. SOMA HAPA Maneno Ya Mauzo Hayafanani Na Maneno Ya Kawaida....
Kuna maneno yanagusa hisia.
Yanazima hofu.
Yanachochea tamaa.
Yanasisimua akili.
Mfano halisi:
Badala ya kusema: "Hii ni kozi ya ujasiriamali," sema:
"Hii ni silaha ya kutoka kwenye presha ya kukopa kila mwisho wa mwezi."
Badala ya kusema: "Hii ni ofa ya bei nafuu," sema:
"Kabla bei haijapanda kamata nafasi yako leo!"
Maneno ya kuuza hayazungumzii tu faida yanasisitiza maumivu, yanavuruga utulivu, yanatonesha kidonda.
✅ 4. SULUHISHO: Jifunze Lugha Ya Kuuza Sio Kuuza Kama UNAOMBA
Kama unataka kuuza lazima uzungumze kama unaelewa maumivu ya mteja.
Sio lazima uwe na Kiswahili kigumu.
Sio lazima uwe na Kiingereza cha Oxford.
Unachohitaji ni maneno yanayogusa moyo, sio akili.
Na unajua nini?
Hii ni kitu unachoweza kujifunza.
Hatua kwa hatua.
Sentensi kwa sentensi.
🪬 5. Hii Ndio Stori Yangu Nilipoacha Kuandika Kama MWALIMU Na Kuanza Kuandika Kama Mteja...
Miaka kadhaa nyuma, nilikuwa nashangaa.
Ninaandika matangazo, post kali, caption nzuri... lakini kimya.
Siku moja nikakutana na fundi mmoja wa matangazo akanionyesha kitu kidogo tu:
“Acha kuandika kama mtoa taarifa. Anza kuandika kama mtu aliyewahi kuumia.”
Nilianza kubadilika.
Nikatumia maneno yanayouma.
Nikaanza kusimulia stori.
Nikawachokoza watu kwa hisia, sio taarifa.
📈 Ndani ya wiki mbili niliuza mara tatu zaidi ya kawaida.
Leo hii, nafundisha wengine kufanya hivyo.
Kama bado unatumia maneno ya kawaida kujaribu kuuza usishangae kama biashara yako inaendelea kuwa ya kawaida.
Badilisha lugha.
Zungumza kama mtu anayejali.
Gusa maumivu yao.
Chochea tamaa zao.
Sambaza matumaini yao.
Ndipo utaona tofauti ya kweli.
Kujifunza zaidi, wasiliana na 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
https://forms.gle/W4acPufZXjFRYjUt7
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni