Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Unataka Mafanikio? Acha Kuitafuta Siri Kwenye YouTube Ipo Ndani ya Vitabu!

Hapo nyuma,


‎Nilikuwa kijana wa kawaida, nikilala chini, huku nikiamka kila siku kwenda kwenye kazi yenye mshahara mdogo kazi ya kuhesabu saa, si mafanikio.

‎Hali ya kifedha haikuwa nzuri, bili ziliniandama, na ndoto zangu zilikuwa zimejaa vumbi.

‎Siku moja, nikiwa nimechoka sana, nilikuta kitabu cha zamani kwenye kibanda cha magazeti “The Richest Man in Babylon.”

‎Mzee aliyekuwa akiuza gazeti akaniambia, “Hiki kitabu, kimenisaidia sana chukua usome.” Nilitabasamu kwa kejeli.

‎Kitabu? Kitaniokolea nini?

‎Nilikichukua lakini sikukisoma. Nilihisi kama ni kupoteza muda. Kwani vitabu vinaweza kuleta hela? Wiki zikipita, niliona maisha yangu yanazidi kuwa yale yale. Nilianza kujiuliza, “Je, kuna kitu ninakikosa?”

‎Siku moja nikakutana na jamaa mmoja aliyewahi kuwa masikini kama mimi.

‎Alikuwa na biashara tatu, gari kali na alikuwa anatoa mafunzo.

‎Aliniambia maneno yaliyonichoma rohoni:

‎ “Ramadhani, mafanikio ni sawa na jiko yanahitaji kuni. Na kuni ni maarifa.

‎Unapataje maarifa? Kwa kusoma.

‎Vitabu ni mbegu za fedha.”

‎Nikachukua hatua: Nikaweka lengo la kusoma kitabu kimoja tu kila wiki.

‎Sikuamini kama nitaweza, lakini nikaamua kujaribu. Wiki ya kwanza kitabu kimoja.

‎Wiki ya pili kingine. Wiki ya tatu nikaanza kuandika maelezo.

‎Wiki ya nne nilianza kubadilisha maamuzi yangu ya kifedha.

‎Watu walianza kunicheka, “Unajifanya msomi sasa?” Lakini niligundua kitu kila kitabu nilichosoma kilinipa mbegu mpya ya fikra.

‎Nilijifunza kuwekeza, kuandika bajeti, hata kuanzisha mradi mdogo wa kuuza bidhaa mtandaoni.

‎Miezi sita baadaye, nilikuwa nimesoma vitabu 26. Nilijifunza kuhusu tabia za watu matajiri, jinsi wanavyofikiri tofauti, jinsi wanavyotumia fedha kama chombo si kama bwana.

‎Nilianza kuwa na nidhamu, kuweka akiba, na kufikiri kama mwekezaji.

‎Nilipoamua kuacha kazi ili nijiajiri rasmi, nilikumbwa na mashaka.

‎Je, maarifa haya ya vitabu yatatosha?

‎Nilipata hasara mara ya kwanza. Lakini nikakumbuka kilichofundishwa kwenye kitabu cha Failing Forward “Kila hasara ni darasa.”

‎Mwaka mmoja baadaye, nilikuwa na biashara yenye faida ya elfu 50 kwa wiki.

‎Nikaanza kufundisha wengine, nikaandika kitabu, na watu walinilipa kusikia hadithi yangu.

‎Kila hatua ya mafanikio yangu ilikuwa na kivuli cha kitabu nyuma yake.

‎Kusoma vitabu ni uwekezaji mkubwa kuliko hata mtaji wa fedha. Vitabu vinakupa mtaji wa fikra, na fikra ndio huzalisha fedha.

‎Mimi si yule kijana wa kuombaomba tena. Mimi ni mwandishi, mkufunzi, na kocha. Na yote yalianza kwa kusoma kitabu kimoja.

‎Kusoma vitabu si hobi ni daraja la utajiri.

‎Kama una ndoto ya kifedha, chukua hatua leo.

‎Anza na kitabu kimoja tu. Hiyo ndiyo hatua yako ya kwanza kuelekea uhuru wa kifedha.

‎Watu wengi hutafuta njia ya mkato kuelekea utajiri.

‎Lakini njia halisi iko kwenye kurasa za vitabu.

‎Maarifa huzaa maamuzi bora, na maamuzi bora huzaa utajiri.

‎Anzia hapa 👇

‎wa.me/255750376891.

‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Ramadhani Amir,

‎Mwandishi| Mkufunzi Wa Mauzo Yenye MAFANIKIO| Kocha Wa MAFANIKIO Ya Mauzo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection