Kwanini Wateja Hawaji? Dhana Potofu Unazozikumbatia Bila Kujua
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Lucas alikuwa kijana mchanga aliyekuwa na ndoto kubwa ya kuwa mfanyabiashara maarufu jijini Arusha.
Alifungua duka la vifaa vya simu aliweka bidhaa mezani, akapamba maduka, akachapisha vipeperushi, na kila asubuhi aliingia mapema kwa matumaini.
Lakini mwezi ukapita, kisha mwingine.
Hakukuwa na wateja wa kutosha. Alianza kujiuliza:
"Ninajitahidi, mbona wateja hawaonekani?"
Siku moja, akiwa amekaa nje ya duka akiwa amechoka, mzee mmoja mtaalamu wa biashara alikuja na kumwambia:
“Una bidhaa nzuri, lakini si kila anayepita anajua hilo.
Tatizo si bidhaa zako, bali imani zako kuhusu wateja.”
Maneno yale yalimgonga kama radi.
Lucas hakuwa amewahi kufikiri kuwa kuna dhana potofu zinazomzuia.
Lucas alicheka kwa kutoamini:
"Mzee, mimi nimesoma YouTube kila usiku, nimefanya kila kitu!"
Alijisemea:
"Labda biashara haijapangwa kwa ajili yangu.
Labda watu wa Arusha hawapendi kununua..."
Lakini kila siku aliporudi nyumbani na fedha haziongezeki, mioyo ya wazazi wake inavyomuamini, walijua lazima kuna kitu anafanya vibaya.
Ndipo rafiki yake wa zamani, Amina aliyewahi kuhudhuria mafunzo ya MAUZO alimtembelea.
Amina alimwambia kwa sauti ya utulivu:
“Lucas, tatizo lako si bidhaa, bali mtazamo.
Kuna dhana nyingi tunazozikumbatia kama wajasiriamali bila kujua zinatufukuza wateja.”
Akamkabidhi vitabu vya mauzo:
Akasema:
“Soma hiki. Sio tu utaongeza mauzo, utabadilika kabisa.”
Lucas alianza kusoma.
Sura ya kwanza ilimshangaza:
"Wateja hawaji kwa sababu unatangaza bidhaa, badala ya thamani.
Unauza kama unawasihi, badala ya kuwashawishi."
Sura ya pili ilimfunua macho:
"Unatumia lugha ya 'tunakukaribisha' badala ya 'hii itakusaidia kutatua tatizo lako'."
Lucas alianza kuona mambo tofauti.
Akiwa na maarifa mapya, alianza kubadili vipeperushi vyake.
Badala ya kuandika “Karibu Duka La Lucas”, aliandika:
👉 "Pata Kioo Cha Simu Kisichopasuka Hata Ukikidondosha Mara Tatu."
Alianza kuandika hadithi kwenye mitandao.
Akajifunza kutafuta mahitaji ya wateja kabla ya kuuza.
Lakini bado alikumbana na changamoto baadhi ya watu walimcheka, wengine walimpuuza.
Hapo ndipo alikumbuka ushauri wa kitabu:
"Mteja ni kama mpenzi, hapendi kusumbuliwa. Anapenda kuvutwa kwa hisia."
Baada ya wiki sita, Lucas alipata mteja wa kwanza aliyempongeza:
“Uliandika ujumbe wenye kunigusa ndio maana nikaingia.”
Alilia usiku huo, si kwa uchungu bali kwa furaha.
Alijua, amevuka kizuizi kilichokuwa kinamzuia kwa miaka mingi imani potofu.
Mwezi mmoja baadaye, duka lilianza kuwa na msongamano.
Lakini sasa alikumbana na changamoto mpya hakuweza kuhudumia vyema bila mfumo.
Alirudi kwenye kitabu, kwenye sura ya mwisho:
“Mauzo bila mfumo ni kama ndoa bila mawasiliano huwezi kudumu.”
Akatumia mbinu za kitabu kubuni mfumo wa kufuatilia wateja, kurekodi mahitaji, na kutoa huduma bora.
Lucas alianza kuona tofauti kubwa.
Wateja walikuja, na walirudi.
Alikuza biashara, akafungua tawi lingine.
Akaanza kufundisha vijana wengine.
Na kila akisimama kwenye jukwaa kusema:
“Nilikuwa nadhani bidhaa pekee inatosha.
Lakini kumbe mawazo yangu yalikuwa kikwazo kikubwa.”
Leo hii, Lucas ni mshauri wa mauzo.
Akiwa na maduka manne, ana ndoto za kuwa na matawi nchi nzima.
Kila kijana anayemfuata anapata jibu moja:
“MAUZO.”
Lucas hakubadilisha tu biashara alibadilisha maisha yake.
Alijifunza kuwa:
Wateja hawaji kwa sababu hujajifunza jinsi ya kuwavuta kwa kutumia maneno, hisia na thamani wanayoitaka.
Sasa anasema kwa ujasiri:
"Wajasiriamali wengi hawana tatizo la mtaji wana tatizo la fikra zilizopitwa na wakati kuhusu wateja.
Ndio maana hakuna anayenunua."
Kama wewe pia unashangaa “kwanini wateja hawaji?”
Usilalamike tena.
👉 Ingia Hapa 👇
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir
Mwandishi| Mkufunzi Wa Mauzo Yenye MAFANIKIO| Kocha Wa MAFANIKIO Ya Mauzo.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni