Kurasa 10 Tu… Ndipo Nilipotaka Kukitupa Kitabu Dirishani....
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kuna Kipindi.....
Nilijua kabisa kuwa watu waliofanikiwa wanasoma vitabu.
Nikajipa changamoto: “Nitasoma kitabu kimoja kila mwezi.”
Nikaanza na motisha kali, nikakaa vizuri, nikaweka daftari la dondoo.
Lakini… kilichotokea kiliniumiza moyo.
Kurasa kumi za mwanzo nilisoma kwa kasi ya roketi.
Ilikuwa kama ndoa ya mapema yote ni furaha na matumaini.
Lakini ghafla… nikaanza kuchoka.
Nilikuwa nimesoma lakini sikumbuki nilichosoma.
Nikaanza kuchek WhatsApp katikati ya kurasa.
Halafu nikasema: “Labda kitabu chenyewe hakivutii.”
Nikaanza kulaumu kila kitu:
📌 Lugha ni ngumu
📌 Mistari ni mingi
📌 Sina muda
📌 Mbona ni boring?
Nikahifadhi kitabu kwenye droo.
Na changamoto yangu ya mwezi? Ilikufa siku ya pili.
Nikamkuta kijana mmoja kwenye YouTube, anasema:
"Tatizo si wewe. Tatizo ni mfumo wa kusoma uliorithishwa.
Vitabu vinahitaji mbinu, si nguvu za mabega."
Nikamsikiliza hadi mwisho.
Akasema: "Watu huchoka baada ya kurasa 10 kwa sababu hawajasoma kwa malengo, hawajaandaliwa kiakili wala kihisia."
Nikachukua kitabu kingine, lakini sasa kwa njia mpya:
✅ Nikaandika kwa nini nakisoma
✅ Nikagawanya kusoma kwa dakika 10 tu
✅ Nikawa nasoma sehemu yenye utulivu
✅ Nikaanza na sura ya kuvutia kwanza (sio mstari wa kwanza tu wa mwanzo)
Na ghafla… nikagundua siri.
Wengine waliniambia: “Kama huchangamki mwanzo, acha tu.”
Lakini mimi niliendelea.
Nikakutana na wasomaji Telegram na WhatsApp, tukawa tunasoma pamoja.
Kila mtu alikiri: “Kurasa 10 za mwanzo huwa ngumu kwa kila mtu!”
Sio wewe peke yako.
Siku moja niliamua kusoma kitabu kigumu kinachojadili fedha.
Kilikuwa na maneno magumu, namba, na historia nyingi.
Nilitaka kukiacha.
Lakini nikajiambia: "Nitasoma kurasa 5 tu leo, 5 kesho."
Mwishoni, nilikimaliza.
Na matokeo? Yalinibadilisha!
Nikagundua kuwa:
📌 Kusoma ni mazoezi ya akili.
📌 Sio kila kitabu ni cha kusoma mwanzo hadi mwisho.
📌 Hakuna ubaya kusoma sehemu tu ya kitabu.
📌 Mbinu bora hufanya kusoma kuwa safari ya kufurahisha.
Niliamua kusaidia wengine wanaohisi kama mimi.
Nikaandika post: “Kurasa 10 Si Kiama. Ni Geresha Tu Ya Mwanzo.”
Watu wakaanza kuniandikia:
"Asante. Umeniondolea hatia ya kujiona mvivu.”
Mimi sasa ni msomaji wa mbinu, si nguvu.
Nikisoma, najua kwa nini nasoma, najua lini niachie, na najua lini nitafakari.
Situmii tena kusoma kama adhabu ni safari ya maarifa.
Nikuambie ukweli mmoja tu:
Kama unachoka baada ya kurasa 10, hauko peke yako lakini pia hujachelewa kubadilika.
Kuna njia, kuna mbinu, kuna mwanga.
Na ikibidi… usianze na kitabu kizima anza na ukurasa mmoja tu kwa moyo wote.
Kujifunza zaidi na kuungana na wenzako makini waliodhamiria kuleta mapinduzi Makubwa,
Kupitia usomaji wa vitabu,
Basi tuwasiliane kwa simu namba 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Kocha Ramadhan Amir,
Mwandishi | Mkufunzi Wa Mauzo Yenye MAFANIKIO| Kocha Wa MAFANIKIO Ya Mauzo.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni