Kuna Tofauti Gani Kati ya Kusoma Vitabu Halisi na Audiobooks?
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
📘 Sauti Iliongea Nami… Ndipo Nikagundua Nguvu Halisi ya Kusoma
Mimi nilikuwa msomaji wa kawaida sana.
Nilipenda vitabu… lakini muda wa kusoma? Hakuna!
Kazi nyingi, kichwa kiliniuma jioni, mara simu, mara familia.
Vitabu vinanivutia lakini kuvisoma ni kama kujilazimisha.
Nikaanza kujisikia kama nimechoka kuwa na ndoto zisizoendelezwa.
Siku moja rafiki yangu akaniambia:
"Kama kusoma kunakuchosha, kwanini usijaribu audiobook?"
Nilicheka tu.
"Kusikiliza si sawa na kusoma!" Nikasema kwa kejeli.
Nilihisi kama nikisikiliza kitabu, nitakuwa mvivu.
"Hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kusikiliza tu... ni kama kudesa!"
Niliendelea kung’ang’ania vitabu vya karatasi, lakini vingi vikasalia na vumbi kabatini.
Siku moja nikiwa YouTube, nikamuona mtu mashuhuri akisema:
"Audiobooks zimenisaidia kusoma zaidi ya vitabu 50 kwa mwaka."
Nikaguswa. Nikasema:
"Subiri kidogo… Huyu amefanikiwa, na anasikiliza vitabu? Labda kuna jambo hapa."
Nikaamua kujaribu.
Nikapakua audiobook ya “The Magic of Thinking Big.”
Nikaisikiliza nikiwa kwenye foleni, jikoni, hata bafuni.
Kwa mara ya kwanza, nilihisi kitabu kinasimuliwa moja kwa moja ndani ya moyo wangu.
Wengine walinicheka:
"Eti unasoma kwa sikio? Hujui kusoma au?"
Lakini mimi niliendelea.
Nikawa na marafiki wa Telegram na WhatsApp wanaosikiliza pia.
Tukaanza kushirikiana vipengele vilivyotugusa.
Nilijaribu kurudi kwenye vitabu vya kawaida, lakini nikashindwa kuvimaliza.
Nilihisi hatia.
Je, hii ni dalili kwamba naachana na vitabu halisi?
Lakini moyoni nikajiuliza: “Hii ni vita kati ya njia na lengo, sio maadili.”
Nikagundua si njia unayosoma, bali kile unachopata.
Nilianza kuelewa tofauti:
Vitabu vya karatasi vinanifaa nikitaka kuandika, ku-highlight na kufikiri kwa kina.
Audiobooks zinanifaa kusikiliza kila sehemu, kujifunza haraka, na kupata msukumo.
Zote ni muhimu, ila kwa wakati tofauti.
Nimeanza kushauri watu:
"Usilazimishe njia. Tafuta njia inayokufaa kwa kipindi chako cha maisha."
Mmoja akanijibu: “Sikuwahi kumaliza kitabu hata kimoja, lakini sasa nimesikiliza vitabu vitano. Asante!”
Mimi sasa ni msomaji huru.
Sioni aibu kusoma kwa sikio wala kwa macho.
Najua ninachotafuta ni mabadiliko ya ndani si kujionyesha kwamba nimesoma.
Leo, nakuambia wewe msomaji wangu:
Sio njia unayotumia kusoma, bali ni jinsi unavyobadilika kwa kile ulichosoma.
Ikiwa vitabu vya karatasi havikubebi kwa sasa, usijilaumu jaribu audiobook.
Kilicho muhimu ni kujifunza, si kuonekana unajifunza.
Niandikie Hapo Kwenye Comment Unataka Kitabu Gani,
Au Tuwasiliane Kwa Namba 0750376891.
Useme Unataka Kitabu Gani.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhan Amir
Mwandishi Wa Vitabu| Mkufunzi Wa Mauzo Yenye Matokeo | Kocha Wa Mafanikio Ya Mauzo
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni