‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...

 ‎ Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. ‎ ‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... ‎ ‎Nilikuwa nimehitimu shule. ‎ ‎Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. ‎ ‎Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” ‎ ‎Sikupata kazi niliyoitegemea. ‎ ‎Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" ‎ ‎Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain ‎ ‎Nikaanza kujiuliza: ‎ ‎"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" ‎ ‎Nikapuuzia. ‎ ‎Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. ‎ ‎Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. ‎ ‎Mbona havifundishwi shuleni? ‎ ‎Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? ‎ ‎Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: ‎ ‎"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." ‎ ‎Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” ‎ ‎Akaniongeza na kingine:  ‎ ‎“The 7 Habits of ...

‎Kijana Aliyekataa Kuishi Kawaida Safari Ya Kivuli Mpaka Kuangaza Dunia...

Hapo Mwanzoni mwa mwaka 2009.

‎Kulikuwa na kijana mmoja wa kawaida aliyeishi katika kijiji cha mbali,

‎ Hakujulikana, na hakuwa na chochote cha kipekee, na kila mtu alimwona wa kawaida sana.

‎Lakini moyoni mwake, kulikuwepo na ndoto kubwa: kuwahi jukwaa la dunia na kuacha alama.

‎Siku moja, aliona tangazo dogo la kozi ya maarifa mtandaoni. 

‎Alihisi mwito ule wa sauti ya ndani iliyomwambia, “Hii ni nafasi yako.”

‎Aliamua kujiunga, licha ya upinzani wa familia na marafiki waliomcheka:

‎Nakumuuliza mara kwa mara,

‎*Utasoma vitabu? Utalisha familia na karatasi?*

‎Safari yake ilianza  usiku mwingi bila usingizi, video bila bundles, vitabu vya PDF alivyovichapa kwa hela ya chakula.

‎Alijifunza kuhusu fedha, biashara, saikolojia ya mafanikio…

‎Alipojaribu mara ya kwanza kuanzisha biashara ilifeli.

‎Mara ya pili – wateja walimkataa.

‎Mara ya tatu – watu wakaanza kumuuliza,

‎*Unawezaje kuelewa hivi vitu kwa undani hivi?*

‎Miaka miwili baadaye, kijiji kizima kilimwalika kuwa mgeni rasmi wa tamasha la maendeleo.

‎Jukwaani alisimama, si tena kijana wa kivuli, bali shujaa aliyeshinda hofu, ukosoaji na umasikini.

‎Na sasa, kupitia kitabu chake kipya, anafundisha wengine kuanza safari yao ya kishujaa.

‎Anyway, kama bado hujapata kitabu hiki wasiliana na 0750376891.

‎Karibu.

‎Rafiki Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir,

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?