Copywriting; Jinsi Nilivyowavuta Wateja Wa Kulipia Bila Kuomba Kazi Siri Inayobadilisha Game
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kuna wakati nilichoka.
Kuchoka kuomba kazi kila mahali.
Kila inbox nikiandika “Naweza kusaidia na hii…”
Kila jibu likiwa “Tutakujulisha.”
Na mengine hata hayajibu.
Nikasema basi!
Na hapo safari yangu ikaanza.
Siku moja nikaandika post moja.
Ya ukweli.
Iliyojaa maumivu.
Ilikuwa story yangu.
Sio kusales.
Sio kujiuza.
Ilikuwa ukweli – "Nimechoka Kuomba Kazi."
Watu wakacomment.
Wengine wakashare.
Wateja wakaanza kuni-DM.
Nikagundua kitu:
Watu hawavutiwi na cheti,
Wanavutwa na hisia zako.
Watu hawakumbuki huduma yako,
Wanabeba story yako.
Nikaanza kuchora hadithi.
Kila post – story.
Kila content – emotions.
Kila status – ladha.
Sio kuomba kazi,
Ni kuwaonesha maisha yako.
Nilikuwa na shaka.
"Nikiandika sana, wataniona nalilia kiki?"
Lakini guess what?
Wale waliodhani hivyo, hawakunilipa hata elfu moja.
Lakini yule mmoja…
Aliyenisoma kimya kimya kwa wiki tatu,
Akanitumia email moja:
“Hi, I’ve been following your posts. You’re exactly who we need. How much do you charge?”
Na hivyo ndivyo ilivyoanza.
Sikuandika proposal.
Sikupeleka CV.
Sikuomba kazi.
Niliandika ukweli wangu.
Nikaonyesha thamani kwa stori.
Wateja wakaanza kuja wenyewe.
Wengine wakasema,
“Nimekuwa niki-screen freelancers 5,
lakini kuna kitu cha kipekee kwako.”
Wakawa wateja.
Wa kulipia.
Wa kurudi tena na tena.
Leo nakwambia hivi:
Acha kubembeleza kazi.
Acha kudanganya CV.
Tengeneza hadithi zako.
Onyesha thamani bila kujigamba.
Weka ladha ya utu kwenye kila unachofanya.
Sio kila mtu atakuelewa.
Sio lazima uvutie kila mtu.
Unachotaka ni wale walio sahihi.
Unataka wateja wa kulipia?
Waache waje kwa moyo wao.
Wavute kwa hisia.
Wavute kwa thamani.
Wavute kwa hadithi.
Wateja sio wajinga.
Wanapenda ukweli.
Wapatie ladha ya ubinadamu.
Na utawavuta – bila kuomba kazi.
✅ Unataka nikusaidie kuandika hadithi zako za kuvutia wateja wa kulipia? Ni-DM. Usiogope, unaanza hapa!
Namba Ni 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir| Copywriter|
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni