Biashara Yako Haifi kwa Kukosa Wateja… Inakufa kwa Jinsi Unavyowasaka!
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mwaka 2021...
Kassim alikuwa na bidhaa kali.
Duka safi.
Bei poa.
Huduma bomba.
Lakini hela hazikuingia.
Wateja walikuwa wachache kama chai ya asubuhi.
Kila mtu alimwambia:
“Tulia tu, ipo siku watakuja.”
Lakini siku hazikuja.
Wiki zikapita.
Mwezi ukapita.
Deni likaongezeka.
Siku moja jamaa mmoja alimchombeza:
“Kaka, biashara si kusubiri wateja. Biashara ni kuwasaka lakini kwa akili.”
“Leo ukikaa tu, kesho utauza shelves zako.”
Maneno yale yakamgonga.
Akaanza kutafuta njia ya kuwasaka wateja kisomi.
Sio kwa mabango.
Sio kwa post za kubahatisha.
Bali kwa mfumo wa kufuatilia kila aliyeonyesha interest.
Akaelewa kwamba:
✅ Wateja hawatokei tu – unawavuta.
✅ Wateja hawaombi – unawasha kiu.
✅ Wateja hawajirudii – unawakumbusha.
✅ Wateja si marafiki – wanataka Thamani kabla ya kutoa hela.
Usipowasaka, utawabaki kuwaangalia kwa macho.
Wateja wako hawajaisha wamechoka kusumbuliwa hovyo.
Usakaji si kudandia inbox ni kuingia kwenye akili zao bila kupiga kelele.
Kama hujui kuwasaka, basi unawasukuma kwa washindani wako.
Biashara bila usakaji ni kama mpenzi bila SMS, penzi linakufa kimya kimya.
Leo Kassim anasema:
“Siku niliyojifunza kusaka wateja kwa akili…
Ndiyo siku biashara yangu ilizaliwa upya.”
Kujifunza zaidi, tuwasiliane kwa 0750376891.
Karibu.
Ramadhani Amir.
Mwandishi| Mkufunzi Wa Mauzo Yenye MAFANIKIO| Kocha Wa Mafanikio Ya Mauzo.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni