Unapuuza Silaha Inayoweza Kukutoa Kwenye Umasikini, Kila Siku Bila Kujua!...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu Mpendwa,
Wewe unateseka.
Kila siku unakimbizana kutafuta hela.
Lakini maisha yako bado ni yaleyale.
Unajua kwanini?
Kwa sababu unapuuza silaha moja rahisi sana: KITABU.
Ndiyo, kile kitu unachokiona kama vya wasomi pekee.
Kile unachosema “Mimi si mtu wa kusoma.”
Hicho ndicho kinachokuweka hapo ulipo.
Vitabu ni Siri ya Mafanikio.
Zimebeba akili za matajiri, wabunifu, na watu waliokwishapitia ulichonacho.
Lakini wewe unapita navyo kama takataka.
Hebu jiulize...
Kila siku unatumia masaa 4 kwenye TikTok, Insta, na kuangalia video za utani.
Lakini dakika 15 kusoma kitabu?
Huipati!
Halafu unataka utajiri...
Unataka biashara izae...
Unataka maisha ya mamilionea...
Lakini hutaki kujenga ubongo wa kimamilionea!
Huwezi kuwa tajiri kwa akili ya kupenda starehe na uvivu wa maarifa.
Wewe ndiye unajizuia mwenyewe!
Wengi wanasema, “Aaah vitabu havisaidii.”
Huo ni uongo uliopakiwa kwa ujinga.
Vitabu vimewabadilisha watu:
Waliokuwa maskini kabisa leo ni mabilionea.
Waliokuwa hawajui hata kuandika leo wanatoa mihadhara duniani.
Hutahitaji kusoma kila ukurasa wa kila kitabu.
Dakika 15 tu kila siku… zinatosha kukuingiza kwenye dunia ya tofauti.
Kwa hiyo ukisema vitabu havisaidii,
unajikata miguu mwenyewe.
Sasa sikiliza:
Anza leo.
Chagua kitabu kimoja tu cha maarifa – hata iwe “Nguvu Ya Buku.”
Kaa kimya.
Soma dakika 15 kila siku.
Andika pointi tatu kila siku.
Kisha, fuata unachojifunza.
Miezi 3 tu utashangaa:
Fikra zako zitakuwa zimebadilika,
na mafanikio yataanza kusogea.
Vitabu sio tu maneno, ni silaha.
Silaha ya akili.
Silaha ya kupasua umasikini.
Silaha ya kutoka utumwa wa madeni.
Kuna kijana mmoja mtaani kwetu alikuwa analala kwa bibi yake.
Maskini hadi viatu havina mguu.
Siku moja akapewa kitabu:
"Think and Grow Rich" – Tafsiri ya Kiswahili."
Akasema, “Ah, ngoja nisome tu kuona.”
Alichofanya?
Kila siku dakika 15.
Akaanza kuandika ndoto zake.
Akaanza kuuza vitu vidogo vidogo.
Leo?
Ana kampuni yake ya online.
Anasaidia vijana wengine kusoma vitabu.
Na kila wiki anakumbusha watu:
“Sikufika hapa kwa connections, nilianza na kitabu.”
Unakaa kulalamika maisha magumu,
wakati silaha iko mezani mwako!
Usiipuuze.
Usicheze na vitabu.
Usicheze na maarifa.
Anza leo,
soma dakika 15 tu kila siku.
Utaona tofauti ndani ya miezi michache.
“Watu wanaofanikiwa si wa ajabu ni watu waliotumia silaha unayoipuuza kila siku: KITABU.”
Unataka kubadilisha maisha yako?
Anza na kurasa moja tu leo.
Anyway, Kama Unataka Vitabu Vizuri,
Wasiliana Na 0750376891.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
0750376891.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni