Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

🔥 Ukipitwa Na Vitabu Hivi 5 Kabla Ya Miaka 30


🔥 Ukipitwa Na Vitabu Hivi 5 Kabla Ya Miaka 30,


Maisha Yatakunyoosha Sana.


Kakaa/ Dadaa Yangu ,


Kuna ukweli mchungu, lakini nitakuambia tu:

Kama hujasoma vitabu sahihi mapema, maisha yatakusoma wewe.


Wengi wanateseka si kwa sababu hawana akili.

Wanateseka kwa sababu hawana maarifa.

Hawajui wapi pa kuanzia.

Wamebanwa na madeni.

Wana mahusiano yanayowaumiza.

Wanadanganywa kirahisi.


Na yote hii?

Inatibika kwa kujifunza kitu kimoja: KUJIELEWA.


Na njia rahisi ya kujielewa?

Ni kusoma vitabu ambavyo vinafungua macho kabla ya miaka 30.


Sababu?

Miaka 30 ni kama mlango – ukivuka bila maandalizi,

Unazama.



Sasa fikiria...

Miaka 35 umefika,

Huna kazi ya kueleweka.

Umeoa/umeolewa vibaya.

Rafiki zako wote wanaendelea, wewe unarudi nyuma.


Unaanza kusema, “Dunia haina haki.”

Lakini tatizo si dunia...

Tatizo ni ulipoteza muda mwingi bila kujitengeneza mapema.


Ulisema vitabu ni vya wasomi.

Ulisema huna muda.

Ulisema hutaki kusoma, unataka hela.


Sasa uko wapi?

Umelogwa na uvivu wa maarifa.


Wengi hufikiri mafanikio ni bahati.

Eti kuna mtu aliangukiwa tu na maisha mazuri.


HAPANA.

Mafanikio ni mfumo.

Na mfumo huu unajengwa kwa kujifunza hatua kwa hatua.


Sio lazima usome vitabu 100.

Lakini kuna vitabu 5 tu vya kwanza vinavyoweza kugeuza akili yako.

Vikikupita, unaweza potea kabisa.


Sasa ngoja nikudondoshee hivi vitabu 5

Vya kuchoma mafuta usiku ukiwa navyo.


1. Rich Dad Poor Dad – Robert Kiyosaki

👉 Kitakufundisha tofauti ya kutafuta pesa na kuijenga.

👉 Utajifunza jinsi matajiri wanavyofikiri.


2. The 7 Habits of Highly Effective People – Stephen R. Covey

👉 Tabia 7 za watu wanaobadilisha dunia.

👉 Inaweka akili yako kwenye mstari.


3. How To Win Friends & Influence People – Dale Carnegie

👉 Mahusiano ni kila kitu.

👉 Ukijua kuzungumza na watu, milango hufunguka.


4. Think and Grow Rich – Napoleon Hill

👉 Hili ni somo la nguvu ya kufikiri.

👉 Linakufundisha kutengeneza mafanikio kichwani kabla hayajatokea.


5. Atomic Habits – James Clear

👉 Mafanikio ni matokeo ya tabia ndogo ndogo kila siku.

👉 Kitabu hiki kitakuwekea ratiba ya ushindi.


Hapo nyuma...


Niliwahi kukutana na kijana mmoja, anaitwa Chidi.

Alikuwa fundi simu.

Anapata elfu mbili, elfu tano kwa siku.


Siku moja akaniuliza, “Bro, nifanyeje niache kuhangaika hivi?”


Nikampa kitabu cha Rich Dad Poor Dad.

Siku 3 baadaye, alinipigia,

Akanambia:

“Nimegundua nimekuwa maskini kwa sababu ya fikra zangu.”


Leo hii Chidi anamiliki duka la vifaa vya simu.

Anafundisha vijana wengine.

Anaandika kitabu chake.


Alianza na kitabu kimoja.

Na hakurudi nyuma tena.


Kwahiyo,

Usingoje miaka 30 ikukute ukiwa kipofu wa akili.

Chukua vitabu.

Soma.


Kumbuka:

“Maisha ni mepesi kwa waliotayari, na magumu kwa wavivu wa maarifa.”



Muhimu; Kama Bado Hujajiunga Na Wenzako Makini Basi Piga Simu 0750376891.


Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,


Mkufunzi Ramadhan Amir 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection