Soma Dakika 15 Kila Siku: Njia Rahisi Ya Kuvunja Umasikini Na Kujenga Utajiri...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu...
Unalala na simu mkononi.
Unamka na WhatsApp, Insta, na bet.
Hujawahi kukaa chini usome dakika 15 hata siku moja.
Na bado unajiuliza, “Mbona maisha hayaendi?”
Sasa sikia…
Watu wengi wanadhani utajiri unatokana na bahati.
Au kuwa na baba tajiri.
Au kufungua biashara kubwa ghafla.
Hawajui siri moja ya ajabu:
Dakika 15 tu za kusoma kila siku zinaweza kubadili kila kitu.
Sio lazima usome vitabu vigumu kama vya sayansi.
La hasha.
Unaweza kusoma kuhusu pesa, biashara, akili, au tabia za mafanikio.
Ni kama kuchoma mafuta polepole lakini mwisho gari linafika mbali sana.
Lakini unajua kinachoumiza zaidi?
Watu wanaosema “mimi sibadiliki kwa kusoma!”
Wanasema hivyo wakiwa broke.
Wakiwa wamechoka na maisha.
Wakilia usiku, wakicheka mchana.
Wanataka pesa, heshima, uhuru…
Lakini hawako tayari kusoma hata ukurasa mmoja kwa siku.
Wanakataa kusoma lakini wanakubali kuumia.
Wanachoka kusubiri neema ya ghafla, wakati wenyewe wamekata neema ya maarifa.
Kuna uongo mkubwa sana unaenezwa mtaani:
Eti “vitabu havisaidii tena.”
Huu ni mtego.
Unaangusha wengi.
Kwa sababu ukweli ni huu:
Watu matajiri wanajifunza kila siku.
Wanasoma.
Wanasikiliza.
Wanatafuta maarifa mpya kila siku.
Wewe unapoacha kusoma, unachagua kubaki nyuma.
Kwenye giza la umasikini, la kutegemea wengine, la kupotea.
Sasa sikia suluhisho la kweli:
Soma dakika 15 kila siku.
Ndiyo. Sio saa nzima.
Sio kitabu kizima.
Dakika 15 tu.
Soma kuhusu:
Jinsi ya kutengeneza kipato
Namna ya kudhibiti matumizi
Tabia za watu waliowahi kufanikiwa
Kwa mwezi mmoja, utashangaa akili yako inavyobadilika.
Kwa miezi sita, utashangaa wallet yako.
Kwa mwaka mmoja, watu watakuuliza “ulilogwa na nani?”
Nimkumbushe Mwanafunzi mmoja anaitwa Mussa.
Alikuwa anauza vocha Kariakoo.
Kila siku, jua kali, kazi nyingi, pesa ndogo.
Akanunua kitabu cha Nguvu Ya Buku.
Akaamua kusoma dakika 15 kila siku.
Akajifunza kuhusu kuweka akiba, kuwekeza buku, na kufungua biashara.
Miaka miwili baadaye, ana duka lake mwenyewe.
Anauza vocha kwa jumla.
Na analipia dada yake chuo.
Wakati wenzake walikuwa busy na michezo ya simu,
Yeye alikuwa busy kuongeza maarifa kichwani.
Leo?
Anasema hivi:
“Siri ni dakika 15 tu za kusoma. Zilinigusa zaidi ya pesa ya bahati nasibu.”
Sasa Ni Zamu Yako…
Utasema nini miaka mitatu ijayo?
"Nilijaribu kusoma na maisha yangu yakabadilika?"
Au
"Nilikuwa busy na Tiktok, sasa nalia mtaani?"
Chagua leo.
Soma dakika 15 kila siku.
Anza na vitabu kama Nguvu Ya Buku, Siri Za Mafanikio, au Jinsi Ya Kudhibiti Matumizi.
Dakika 15 tu.
Zinaweza kuwa tiketi yako ya kutoka kwenye umasikini.
Kama Unataka Vitabu Vizuri,
Tuwasiliane Kwa Kupiga Simu Au Kutuma Ujumbe Kwenda 0750376891.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
#NguvuYaMaarifa
#Dakika15InawezaKubadiliKilaKitu
#NguvuYaBukuToto
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni