🔥 Mambo 7 Unayojifunza Kwenye Vitabu Ambavyo Hukufundishwa SHULENI 🔥...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Alizaliwa na Kuishi Maisha ya Kawaida Sana…
Anaitwa Jumanne. Mtoto wa pili kwenye familia ya watoto saba. Baba mchomeaji vyuma, mama muuza maandazi.
Aliishi maisha ya kujisitiri, hakuwa na nguo za bei, wala viatu vya kuvutia.
Alipomaliza kidato cha nne, hakupata nafasi ya kuendelea na masomo si kwa sababu hakufaulu, bali kwa sababu hakukuwa na ada.
Akiwa nyumbani, kila siku ilimchoma moyo kuona wenzake wakisonga mbele. Hakukuwa na ajira, wala mtu wa kumshika mkono.
Ndoto zake zilianza kuzama polepole. Alianza kuamini pengine maisha haya ni ya waliozaliwa na bahati.
Lakini Mambo Yalianza Kubadilika Siku Aliyopewa Kitabu Kimoja.
Siku moja, jirani yake alimpa kitabu kiitwacho NGUVU YA VITABU.
“Jaribu kusoma hiki Kitabu,” alisema yule jirani, “Hata kama huendi shule, akili yako bado inaweza kuelimika.”
Kwa mashaka na shingo upande, Jumanne alianza kusoma. Kurasa za kwanza zilimkumbusha thamani ya muda, nguvu ya kujifunza, na umuhimu wa nidhamu binafsi.
Aligundua kuwa kuna mambo ambayo shule haifundishi, kama vile:
1. Namna ya kujiongoza bila kusukumwa.
2. Jinsi ya kujiamini hata unapokataliwa.
3. Mbinu za kutafuta maarifa nje ya darasa.
4. Kujenga nidhamu ya kufanya vitu hata kama huna motisha.
5. Jinsi ya kushughulika na fedha ndogo.
6. Nguvu ya kuanza na kilicho mkononi.
7. Namna ya kuvumilia hadi mafanikio yatokee.
Akaanza Maisha Mapya Kwa Kuanza Kidogo Sana.
Alianza kuuza maji baridi kwenye stendi ya daladala. Watu walimcheka, lakini kila siku alisoma kurasa chache kabla ya kutoka.
Alitumia maarifa yale kujiendesha kibiashara. Alijifunza jinsi ya kutunza pesa, kuwahudumia wateja, na kufikiri kama mtu anayejenga biashara.
Mambo Hayakuwa Rahisi.
Mara kadhaa alikatishwa tamaa. Aliibiwa, alifukuzwa kwenye maeneo ya kuuza, hata wazazi wake walimwambia "anza kutafuta kazi ya mshahara mdogo tu uoe ukae."
Lakini moyoni mwake, alikuwa tayari ameshaamka. Alikuwa na maarifa ambayo hakuwahi kufundishwa na mwalimu yeyote, bali kitabu.
Leo Hii, Jumanne ni Mfanyabiashara Mdogo Mwenye Dira Kubwa.
Anamiliki duka la vifaa vya ujenzi na kiosk ya chakula.
Anajitolea kuwasaidia vijana wasio na mtaji kwa kuwapa mafunzo ya kujitegemea. Mara kwa mara huwatembelea wanafunzi mashuleni na kuwaambia:
"Shule ni muhimu… lakini vitabu vinaweza kukufundisha maisha ambayo darasa halijawahi kuyagusa."
Na Wewe Unaweza Kuanzia Hapo Ulipo.
Usingoje mwalimu au ajira. Anza kusoma. Anza leo.
Kwa sababu, kama alivyogundua Jumanne:
“Maarifa yakiingia kichwani, maisha huanza kubadilika.”
📘 Pata nakala ya vitabu vyenye maarifa ya maisha.
Usome. Ubadilike. Ushinde.
Kupata Kitabu Hiki Na Vitabu Vingine Mzuri,
Piga Simu au Tuma Meseji Kwenda 0750376891.
Karibu.
Kutoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
0756694090.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni