Jinsi Ya Kumwambia Mteja Bei Kubwa Bila Kumtisha, Kumkera au Kumkimbiza
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
🧠 “Kaka, Usiwahi Kumwambia Mteja Bei Moja kwa Moja Kama Unaogopa Kuku!”
Unataka kuuza, siyo kuomba msamaha.
Lakini mara nyingi, unapoangalia uso wa mteja…
Unamwambia bei yako, alafu uso wake unabadilika kama vile umetaja jina la ex wake.
👉🏽 Halafu anasema:
“Hiyo ni bei ya mwisho?”
“Aaah… si unishushe kidogo?”
“Kwa hiyo ni hii tu elfu 80?”
“Kwa nini ni ghali hivyo?”
Na hapo ndipo moyo wako unadondoka miguuni.
Unaanza kujitetea.
Unapunguza bei.
Unaua biashara yako mwenyewe.
Lakini usijali. Leo naenda kukupa SUMU YA KIUMBE HAI... Anchoring.
Ukweli ni kwamba sio Bei..
💥 Tatizo Sio Bei Yako – Tatizo ni Jinsi Unavyoiwasilisha
Kuna namna tatu za kuua mauzo:
1. Kumpa mteja bei ghafla kama kombora.
2. Kumpa bei bila sababu yoyote.
3. Kumpa bei huku unatetemeka.
Wateja hawachukii bei.
Wanachukia BEI ISIYOELEWEKA.
👉🏽 Ukimpiga na bei ya 150K bila maandalizi,
Anaona kama unamchuna.
Lakini ukiweka msingi, bei hiyo hiyo inageuka kuwa bahati.
Hapo ndipo ANCHORING inafanya kazi kama ushirikina wa kihalali.
🔥 Sikiliza Nikwambie Kwa Uchungu.
Ni maumivu gani utayapata pale unapomtajia mteja bei ya bidhaa yako ya milioni moja…
Alafu anakushika bega na kukuambia:
“Sijui kama utanielewa, lakini sina hata elfu hamsini.”
Yaani ni kama umemwambia bei ya rocket kwenda Mars.
Hapo inakuuma.
Unajuta kumwambia bei kabisa.
Unaanza kusema, “tungeongea tu kwanza…”
Too late. Ameenda.
Kwahiyo...
Usiwahi tena kusema bei kwa pupa.
Badala yake:
👉🏽 Weka bei kubwa mwanzoni hata kama hauuzi kwa hiyo bei.
Mfano:
“Kama ungenunua hii huduma kwa kampuni zingine, ungeweka laki tano hivi…
Lakini sisi tunapenda watu wanaothubutu mapema.
Sisi tunaiweka kwa 190,000 tu.”
Hapo mteja anaona BEI YA 190K SIYO GHARAMA NI OPPOTUNITI.
Na hiyo ni nguvu ya Anchoring.
Kwahiyo...
Unapomwambia mteja bei ya bidhaa yako,
Usianze na bei yako ya mwisho.
Anza na kitu kikubwa, kikali, kinachoshangaza.
👉🏽 Create Shock Value.
Mfano huu umewahi kufanya watu walie kwa furaha:
> “Unajua hii ni sawa na kununua gari la Vitz mwaka 2018.
Ina nguvu, iko na thamani, na haiharibiki ovyo.
Wengine wanaiuza hadi 250K…
Lakini kwako leo, 98,000 tu.”
Kwa hiyo mteja anaona kama ameokoa pesa.
Na bado amepata kitu cha maana.
Kuna jamaa ninamfundisha copywriting.
Anauza coaching ya kuanzisha biashara.
Alikuwa anatoa bei moja kwa moja: “Ni 150,000.”
Wateja walikuwa wanamkimbia kama ana COVID.
Akaja kwangu na macho mekundu.
Nikampa ANCHOR.
Akarudi sokoni.
Sasa anasema:
“Mafunzo haya nimeyafanya kwa watu waliolipa hadi laki nane.
Lakini kwa sababu nakutaka uanze mapema,
Naamini ukiyafuata utakua mmoja wa walionufaika
Nitakuachia kwa 150,000 tu.”
Matokeo?
Watu wanamlipa kwa furaha.
Wanajisikia kama wamepata dili la karne.
📌 Usisahau: Anchoring Inabadilisha Hisia ya Bei
🔑 Mteja hapimi bei.
Anapima thamani anayohisi kulingana na reference aliyowekewa.
Ukampa bei ghafla atapima kwa akili ya hofu.
Ukampa ANCHOR atapima kwa akili ya thamani.
Zingatia....
✅ Usianze na bei ya kweli.
✅ Weka bei kubwa kama mfano.
✅ Sema sababu ya punguzo.
✅ Mlete mteja kwenye bei yako halisi kama zawadi.
✅ Muache atabasamu, aseme: “Kwa bei hii? Nimepata kitu!”
Wewe ni Mjasiriamali, siyo Muombaji.
Bei yako ina thamani.
Iwasilishe kwa ubunifu.
Tumia anchoring kila siku,
Na utaanza kuuza kama mwendawazimu mwenye neema!
Incase bado hujajiunga na wenzako makini basi nafasi yako hii hapa 👇
Piga au Tuma meseji kwenda 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni