Je, Vitabu Vinaweza Kuondoa Msongo wa Mawazo?....
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu,
Bado namkumbuka....
Alikuwa Hana Kitu. Sio Hela. Sio Mtaji. Sio Tumaini.
Jina lake ni Salma. Msichana wa kawaida kabisa kutoka familia ya kipato cha chini maeneo ya Mbagala.
Baada ya kumaliza chuo kwa tabu, alipambana kutafuta kazi kwa miaka miwili bila mafanikio.
Polepole, akaanza kupoteza matumaini.
Kila siku aliamka akiwa na hofu, akilala na mawazo. Alianza kujitenga na watu, hakupokea simu, na hata chakula kilimchosha.
Msongo wa mawazo ukaanza kula akili yake taratibu.
Kila Kitu Kilibadilika Siku Aliyoangukia kwenye Kitabu.
Siku moja akiwa kwenye daladala, alimsikia mama mmoja akimsimulia rafiki yake kuhusu kitabu kinachoitwa Nguvu Ya Vitabu.
Salma alijikuta akipata hamu ya kukisoma. Ingawa hakuwa na pesa, aliamua kuuza hereni zake ili kukinunua.
Kurasa za kwanza tu, zilianza kumbembeleza polepole kutoka kwenye giza la mawazo.
Alianza kujifunza jinsi akili ya binadamu inavyoweza kubadilika kupitia maarifa. Kitabu kile kilimfundisha mbinu rahisi za kujituliza, kujenga nidhamu, na kujiamini upya.
Alianza Taratibu... Lakini Akaendelea.
Siku ya kwanza, aliamka mapema na kusoma kurasa chache. Siku ya pili, akaanza kuandika malengo yake. Siku ya tatu, akaamua kuandika blogu kuhusu maisha na afya ya akili.
Ndani ya miezi mitatu, watu walianza kumfuata kwenye mtandao. Waliguswa na namna alivyoeleza safari yake ya kutoka kwenye msongo hadi matumaini.
Alifungua ukurasa wa Instagram, akaanza kutoa ushauri mdogo kwa vijana waliopitia kile alichopitia.
Ilikuwa Rahisi? La.
Kulikuwepo siku ambazo alitamani kurudi kitandani na kulia tu. Kulikuwepo maneno ya watu waliomcheka na kumwita "msomi aliyeishiwa.
Lakini alikumbuka maneno ya kitabu kile:
*Mawazo mazuri ni kama mbegu. Ukizipanda, utavuna maisha mapya.*
Leo Salma ni Taa kwa Wengine.
Anaongoza kampeni mitandaoni ya kusaidia vijana wanaokabiliana na msongo wa mawazo.
Ameandika kijitabu chake cha kwanza. Amewasaidia zaidi ya vijana 5,000 kujifunza namna ya kujenga maisha mapya kwa kutumia vitabu.
Na bado anasema, "Yote yalianza na kurasa chache tu… na moyo wa kujaribu."
Je, Wewe Umeshaanza Safari Yako?
Msongo wa mawazo si mwisho wa dunia.
Wakati mwingine, unahitaji tu kitabu sahihi…
Kuanza tu, kidogo kidogo.
Kama Salma, unaweza kuamka tena.
📘 Pata nakala ya kitabu ‘Nguvu Ya Vitabu’ leo.
Inaweza kuwa mwanzo mpya wa maisha yako.
Anyway, kama bado hujapata Kitabu hiki Piga Simu Kwenda 0750376891.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir,
Kakaa Wa Vitabu.
0750376891
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni