Hivi Umeshawahi Kukuta Mtu Anasoma Kitabu Alafu Anakula Pesa? 😳
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu,
Watu wengi wanasoma vitabu.
Wanaandika mistari.
Wanaweka nukuu kwenye status.
Wanafanya kama wameelewa.
Lakini bado broke. 😥
Bado wanahangaika.
Bado hawajui hela inaingiaje.
Kwa nini?
Kwa sababu hawajui kusoma kwa akili ya biashara.
Hawajui kuchuja hela kwenye kurasa.
Hawajui kugeuza maarifa kuwa mpunga.
Wanasoma kwa ajili ya kufurahia tu.
Sio kutengeneza thamani.
Sio kutatua matatizo ya watu.
Na ndio maana unaona:
Wamesoma sana...
Lakini bado wanaomba airtime.
Wanaomba lift ya kwenda kazini.
Wanapiga status za “Siku moja nitafanikiwa.” 😩
Wamesoma vitabu vya Robert Kiyosaki,
Lakini mpaka leo hawajui difference ya asset na liability kwa vitendo.
Wamepitia Think and Grow Rich,
Lakini bado wanathink tu — hawagrow wala hawarichi!
Kibaya zaidi?
Wanasema: “Mimi ni msomi…”
Lakini hela yao ni ya kushika wiki mbili tu.
Kusoma vitabu ni kama kuchimba kisima.
Lakini kama huna ndoo ya kuchotea,
Kuna faida gani?
Unabaki na kiu tu. 😓
Hii ndio siri:
Maarifa bila matumizi ni kama chakula kisichoingia tumboni.
Utaona, utavutiwa, lakini hautashiba.
Vitabu si vya kukumbuka tu.
Ni vya kubadili tabia.
Ni vya kutafuta njia ya kusaidia wengine — halafu kulipwa kwa hiyo msaada. 💰
Kama unataka kugeuza maarifa kuwa pesa:
1. Soma kwa lengo.
Uliza: “Nani ana shida hii?”
“Naweza kuwasaidiaje kwa haya ninayojifunza?”
2. Chuja maarifa ya biashara.
Tafuta pointi zinazoweza kugeuzwa kuwa bidhaa, huduma, au mafunzo.
3. Anza kidogo.
Tumia kile ulichosoma leo kusaidia mtu mmoja.
Iwapo atafaidika anaweza kukuamini.
Anaweza kukulipa.
Hapo ndipo hela inaanza kutiririka.
Mwaka 2019, kulikuwa na kijana mmoja aliitwa Mussa.
Alikuwa anakaa Mwanza.
Maskini lakini mjanja.
Aliokota kitabu kilichokuwa kimechakaa — Rich Dad Poor Dad.
Akakisoma.
Akaandika pointi 10 muhimu.
Akaanza kuzielezea kwa watu kwenye WhatsApp group.
Watu wakaanza kumuuliza: “Unaweza kutufundisha?”
Hakukataa.
Akaandaa session ya Zoom.
Watu 3 walihudhuria.
Baada ya wiki 2, akawa na watu 20.
Leo, Mussa ana kampuni yake ya kutoa mafunzo ya fedha.
Anaingiza pesa ya maana.
Na yote ilianza na maarifa kutoka kwenye kitabu kimoja.
Soma ili kusaidia.
Saidia ili ulipwe.
Ukilipwa basi vitabu vyako vimekuza biashara ya maisha yako.
Hapo ndo kusoma kunalipa.
Unataka kujua mbinu zaidi za kugeuza vitabu kuwa biashara?
🔥 Tafuta kitabu chetu: “NGUVU YA VITABu” kinapatikana sasa hivi kwa ofa ya bure wiki hii!
Kukipata wasiliana na 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni