Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Siri Ya Kuandika Kwa Lugha Ya Mteja, Si Ya KITAALAMU...

Usipojua hii, matangazo yako yatabaki yanapigwa seen tu.




‎Kakaa/Dadaa Yangu...

‎Kwanini unahangaika kuandika copy kali, lakini hakuna anayejibu?

‎Unatumia maneno mazuri, ya kitaalamu, yenye akili nyingi…

‎Lakini hakuna anayekusikiliza.

‎Unahisi kama unaongea na ukuta.

‎Umeandika “Tunakupa huduma bora za kiubinadamu zenye tija na mchango endelevu…”

‎Mteja anakusoma hivi halafu anasema: “Aaah, nini sasa tena hiki?”

‎Kwa nini?

‎Kwa sababu umeandika kama unaongea na professor.

‎Lakini unamuuzia mama wa kwenye genge.

‎Au fundi mkali wa welding.

‎Au kijana wa boda anayepiga hesabu za maisha.

‎Wao hawasomi ili waone unavyojua Kiingereza.

‎Wanasoma ili wajue “hii kitu itanisaidiaje leo?”

‎Unataka kuuza kwa watu wa mtaani?

‎Basi achana na lugha ya vyuoni.

‎Copywriting ni kuingia kichwani mwa mteja.

‎Na si kwa kuonyesha vocabulary yako.

‎Mteja hajali umeenda shule kiasi gani.

‎Anataka usikie kilio chake.

‎Ukiandika kama daktari wa seminar, unapotea.

‎Mfano:

‎Badala ya kusema “Huduma zetu zinalenga kuongeza ufanisi wa mfumo wa kijamii...”

‎Sema tu: “Tutakusaidia upate hela na maisha yawe rahisi.”

‎Simple.

‎Straight.

‎Inaingia kichwani.

‎Siri ni moja tu:

‎ANDIKA KWA LUGHA YA MTEJA.

‎Fikiria anavyoongea akiwa sokoni.

‎Fikiria analalamikia nini akiwa na rafiki zake.

‎Andika vile anavyoongea.

‎Vile anavyolalamika.

‎Vile anavyouliza maswali.

‎Halafu mpe jibu moja kwa moja.

‎Copy kali sio ya kitaalamu.

‎Copy kali ni ile mtu akisoma anasema:

‎“Aah, huyu jamaa ananielewa sana!”

‎Kuna rafiki yangu mmoja, anaitwa Juma.

‎Mwanaume wa mtaani lakini ana roho ya biashara.

‎Alikuwa anaandika matangazo ya biashara yake ya viatu:

‎“Tunauza viatu vya kisasa vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu…”

‎Wateja hawakumuulizia hata bei.

‎Alikuja nikamfundisha kutumia lugha ya mteja.

‎Leo anaandika:

‎“Unatafuta viatu vya bei poa? Vya kuvalia kazini na mtaani? Hizi hapa!”

‎Wateja wakaanza kumuulizia.

‎Wakaanza kuagiza.

‎Kila post inamletea hela.

‎Hapo ndipo aliniambia:

‎“Bro, kumbe siri ilikuwa ni lugha tu?”

‎Nikamuambia:

‎“Ndiyo. Lugha ya mteja ndiyo silaha ya copywriter wa mtaani.”

‎Usisahau:

‎Watu hawataki kueleweshwa kama watoto wa form one.

‎Wanataka kuhisi:

‎“Huyu jamaa ni kama rafiki yangu, ananielewa.”

‎Ukifika hapo…

‎Matangazo yako hayatapigwa seen tena.

‎Yatapigwa ORDER.

‎Copy kali haijivunii akili yako, bali inainamia akili ya mteja.

‎Bado unataka kuandika kitaalamu? Au unataka kuuza?

‎Kupata Kozi kamili ya Copywriting.

‎Tuma Meseji *NATAKA KOZI YA COPYWRITING*

‎Kwenda 0750376891.

‎Karibu.

‎Hii Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection