Nguvu Ya Simulizi Katika COPYWRITING, Hadithi Zinazouza....
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kakaa/Dadaa Yangu...
Watu wengi wanahangaika kuuza, lakini hawauzi.
Wanabuni ofa, wanapanga bei, wanatengeneza matangazo...
Lakini hakuna anayegusa pochi ya mteja.
Kwa nini?
Kwa sababu wanatumia lugha ya kuuza bidhaa,
Badala ya lugha ya kugusa moyo.
Hawajui kutumia simulizi silaha kubwa kabisa kwenye uandishi wa kuuza (copywriting).
Unakumbuka mara ya mwisho ulisoma hadithi fupi ikakufanya ucheke, ushtuke, au hata utoke na machozi?
Hadithi hiyo ilikufanya uendelee kusoma hadi mwisho, si ndiyo?
Sasa jiulize, kwa nini uliendelea kusoma?
Kwa sababu ilikugusa.
Ilikuelewa.
Iliishi maisha yako.
Hapo ndipo nguvu ya simulizi ilipo.
Simulizi nzuri inakufanya uhisi, utafakari, halafu uchukue hatua.
Na hatua hiyo, mara nyingi, ni kununua.
Simulizi siyo porojo.
Siyo hadithi za kufurahisha tu.
Ni mbinu ya kuwasiliana kwa kina.
Ni njia ya kufundisha bila kuhubiri.
Ni daraja kati ya hisia za mteja na bidhaa unayouza.
Simulizi inayouza haileti lengo moja kwa moja.
Inazunguka taratibu.
Inajenga polepole.
Kisha inampeleka msomaji hatua kwa hatua hadi kwenye uamuzi.
Na kama unaamini unaweza kuuza kwa kutumia maneno ya moja kwa moja pekee,
Bila simulizi,
Basi unaacha pesa mezani.
Hivi Ndivyo Simulizi Inavyobadilisha Kila Kitu...
Unapomweleza mteja jinsi ulivyoteseka na tatizo kama lake…
Halafu ukamwonyesha namna ulivyogundua suluhisho…
Na sasa unamtaka na yeye afaidike…
Anasikiliza.
Anaamini.
Anaamua.
Umeunda uhusiano.
Umejenga imani.
Na sasa uko tayari kuuza bila kushinikiza.
Hapo ndipo copywriting ya kisasa ilipo.
Hapo ndipo wauzaji wakubwa wanapoangukia jackpot.
Wanaandika simulizi.
Nilikuwa na mteja mmoja.
Anaitwa Amina.
Aliuza bidhaa za watoto mtandaoni, lakini kwa muda mrefu hakuuza hata pakiti moja.
Nikamuuliza:
"Unamweleza mteja nini?"
Akasema:
"Ninamtajia bidhaa na faida zake."
Nikamuambia:
"Mbona hujaeleza kwa nini ulianza kuuza hizo bidhaa?
Ulipitia nini hadi ukaamua kusaidia akina mama wenzako?"
Akaandika post moja tu.
Akasimulia jinsi mtoto wake alivyoathirika kwa kutumia bidhaa feki.
Akaelezea hofu aliyopitia kama mama.
Kisha akasema alivyogundua bidhaa bora, na akaapa kuziuza ili kusaidia wengine.
Post hiyo iliposambaa,
Aliuza ndani ya saa tatu.
Wateja walimwandikia:
"Hadithi yako imeniumiza moyo. Nimemkumbuka mtoto wangu. Tafadhali niuzie."
Hapo Amina akajifunza...
Hadithi ni biashara.
Ikiwa bado unaandika matangazo kama fomu ya maombi...
Ikiwa bado unawaambia watu "Nunua sasa!" kabla hujawagusa...
Basi unahitaji kujifunza lugha ya hisia.
Na lugha hiyo ni simulizi.
Hadithi inayogusa, inauza.
Hadithi inayofundisha, inashawishi.
Hadithi ya kweli, inajenga imani.
Anza kuandika kama binadamu, si kama roboti.
Anza kuhadithia.
Anza kuuza kwa hisia.
Na pesa zitafuata utulivu.
Ukihitaji kujifunza jinsi ya kuandika simulizi zinazouza, niandikie
“NIKO TAYARI.”
Kwenda 0750376891.
Karibu.
Makala Hii Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
.webp)
Maoni
Chapisha Maoni