Mbinu Rahisi Za Kusoma, Kuandika Na Kushirikisha Maarifa Uliyojifunza....
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kakaa/Dadaa Yangu.
Watu kibao wanasoma vitabu, wanaangalia video kali za maarifa, wanahudhuria semina kali…
Lakini baada ya siku tatu tu, hakuna kitu wamekumbuka.
Maarifa yote yamepotea kama upepo.
Halafu wakikutana na mtu anayetaka kusaidiwa, wanajikuta wamekauka kama jangwa.
Wewe pia umewahi kujiskia hivo? Kama unaelewa hiyo hali… hii makala ni yako.
Unasoma hadi macho yanachoka.
Unanunua vitabu, unaandika notes, unawasha YouTube hadi bundle zinaisha.
Lakini ukiwaulizwa ulichojifunza… kimya!
Unaanza kurukwa na kujiuliza, “Iko faida gani kusoma kama siwezi kutumia haya maarifa?”
Unajikuta unaacha kabisa.
Unakata tamaa.
Unaanza kuamini kwamba, “Labda mimi sio wa kusoma.
Hii mambo ya maarifa sio yangu.”
Lakini ukweli ni huu:
Tatizo sio wewe.
Tatizo ni mfumo wa kusoma.
Watu wengi wanasoma kama wanapiga mswaki haraka haraka tu.
Hawakumbuki, hawajaandika, hawajashirikisha.
Unasoma tu, alafu unaiweka kando.
Unatarajia kumbukumbu itafanya kazi yenyewe.
Hii ni mbinu mbovu. Inakuteka akili kimakosa.
Sasa sikia mbinu rahisi, lakini kali ajabu:
SOMA - ANDIKA - SHIRIKISHA.
Kwanza, soma kwa lengo usiwe tu unasoma ilimradi usome.
Andika pointi tatu au tano ambazo zimekugusa.
Halafu, shirikisha mtu mwingine andika post, tuma voice note, ama ongea tu na mtu.
Utakaposhirikisha, akili yako inaweka maarifa hayo kwenye kumbukumbu ya kudumu.
Inakuwa mali yako ya kweli.
Unakuwa sio msomaji tu, bali mtumiaji wa maarifa.
Mimi mwenyewe nilikuwa hivi.
Nilikuwa nasoma vitabu vya mamilionea, mafanikio, ubongo… lakini sikumbuki hata sentensi moja.
Nilisoma kitabu kimoja cha watu mashuhuri, siku tatu baadaye nikawa hata sijui nilichojifunza ni nini.
Nikakata tamaa.
Lakini baada ya kuanza kuandika yale niliyojifunza kwenye status, kwenye daftari, na kuwaelezea marafiki…
Boom! Maarifa yakaanza kubaki kichwani.
Nikaanza kuyatumia kwenye biashara.
Nikaanza kuwasaidia watu.
Nikaanza kuaminika.
Sasa hivi, kila kitu ninachosoma kinaleta matokeo.
Kwa sababu nakisoma kwa akili, nakiandika kwa mkono, na nakishirikisha kwa moyo.
Kwahiyo,
Ukitaka maarifa yakusaidie soma kwa lengo, andika kwa uhakika, na shirikisha kwa moyo.
Usisome tu ili uonekane msomi.
Soma ili uishi kile ulichosoma.
Na kumbuka…
Maarifa yasiyotumika, ni mzigo tu wa akili.
Ukiona hii makala imekugusa, usiache shirikisha mtu mwingine leo.
Maana… maarifa tunayoshirikishana ndiyo yanayobadilisha maisha yetu.
Kama Bado Hujajiunga Na Jumuia Ya Wasomaji Wa Vitabu,
Basi Bonyeza Hapa 👇
*https://wa.link/nt2nd8*
Karibu Tuendelee Kuwa Pamoja.
0750376891.
Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

Maoni
Chapisha Maoni