Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Maswali Ya Kujiuliza Kabla Hujaandika Copy Yoyote....

 




‎Kakaa/Dadaa Yangu...

‎Unashika kalamu au keyboard.
‎Unataka kuandika copy kali ya kuuza.
‎Lakini… unaandika tu.

‎Bila kujiuliza lolote.
‎Unatumia nguvu nyingi.
‎Lakini matokeo ni zero.

‎Sasa ngoja nikuambie kitu:
‎Copy yoyote, kabla hujaandika, kuna maswali lazima ujiulize.

‎Hii ndiyo siri ya copy inayoingia hadi kwenye damu ya mteja.

‎Kabla hujaandika neno la kwanza, jipe sekunde tano.

‎Jiulize:
‎“Huyu mtu nampa hii copy, anateseka na nini hasa?”
‎Kama hujui hilo… usiandike hata "Hello".


‎Watu hawasikii hadi waumie.
‎Ukiongelea tu faida, hawaguswi.
‎Lakini ukigusa kidonda…

‎Ukikumbusha vile alivyosota jana...
‎Vile alivyotapeliwa kwa kununua kitu kisichofanya kazi...
‎Ndipo anainama asome hadi mwisho.

‎Copy nzuri haiko huko kuleta faraja tu.
‎Inafungua vidonda.
‎Inawasha moto.
‎Kisha ndiyo inakuja na dawa.

‎Wengi wanaamini kitu kimoja:
‎“Copy nzuri ni ile yenye maneno mengi, ya kizungu mingi, au ya kibiashara sana.”

‎Wamesoma sana, lakini bado wanahangaika kuuza.

‎Ngoja nikuambie ukweli mchungu:
‎Copy haivutii kwa lugha, inavutia kwa hisia.
‎Inachoma moyo.
‎Inazungumza kama rafiki.

‎Sio kama daktari au profesa.

‎Kwa hiyo, acha kuandika ili uonekane mjuaji.
‎Andika ili ueleweke.
‎Na mtu wa kawaida kabisa.

‎Sasa, suluhisho ni kujiuliza haya maswali matatu kabla hujaandika chochote:

‎1. Huyu mtu anaumia wapi? (Shida yake haswa ni nini?)


‎2. Anataka nini kwa nguvu zote? (Ndoto yake ni ipi?)


‎3. Kwanini bado hajapata hiyo kitu? (Nini kinamzuia?)



‎Ukijibu haya, unakuwa na ramani ya moyo wake.
‎Unajua pain yake.
‎Unajua ndoto yake.
‎Na unajua kikwazo chake.

‎Hapo ndipo unaandika copy ya moto.


‎Siku moja rafiki yangu mmoja anaitwa Jay, alitaka kuuza eBook ya biashara.

‎Akaandika copy ndefu.
‎Kizungu kibao.
‎Mafumbo tele.

‎Zero sales. Hakuuza hata moja.

‎Nikamuuliza, “Uliandika ukiwa na nani akilini?”

‎Akasema, “Sijui. Nilikuwa naandika tu ili ionekane ya kitaalamu.”

‎Nikamwambia afanye hivi:

‎Ashike simu. Amkumbuke yule jamaa wa mtaani kwao…

‎Anayetaka kufungua biashara ya kuuza mayai.

‎Amwandikie copy kama vile wanakaa wote kwenye stoo, wanapiga stori.

‎Jay akafanya vile.
‎Copy ikawa rahisi.
‎Inaeleweka.
‎Ina feelings.

‎Week moja baadaye: 32 sales.
‎Hakubadilisha bidhaa.

‎Alibadilisha tu namna ya kuandika.

‎Kwahiyo, Usiandike tu ili uonekane mkali.

‎Andika kama unaongea na mtu anayeumia.

‎Jiulize maswali matatu.

‎Gusa hisia.
‎Toa suluhisho.
‎Halafu copy yako itakuwa siyo tu maneno…
‎Itakuwa nguvu.

‎Na hiyo ndiyo kazi ya copywriter.
‎Kuandika maneno yanayouza bila kupiga kelele.


‎Kama Unataka kuungana na Jay na macopywriter wengine walioliteka soko,

‎Andika ujumbe "NATAKA KUWA COPYWRITER KAMA JAY"

‎Kwenda 0750376891.

‎Karibu.
‎Hii Makala Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir,



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection