Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Jinsi Ya Kugusa Hisia Za Msomaji Kwa Sentensi Ya Kwanza....

 



Kakaa/Dadaa Yangu....

‎Kuna waandishi kibao mitandaoni.

‎Wanaandika vizuri.

‎Lakini makala zao hazisomwi.

‎Unajua kwanini?

‎Sentensi ya kwanza haina mvuto!

‎Haimgusi msomaji popote.

‎Yaani ni kama unamwambia, "Usisome hii makala."

‎Hebu fikiria...

‎Umechukua muda kuandika.

‎Umetafakari kichwa cha habari.

‎Umetafuta picha kali.

‎Lakini msomaji anaishia tu hapo mwanzo.

‎Hajui kilicho ndani.

‎Hasogei kabisa.

‎Unabaki unaumia kimoyomoyo.

‎“Mbona hawasomi makala zangu?”

‎Ni kama kupika pilau halafu mtu anakataa hata kuonja.

‎Wengi hufikiria kuwa sentensi ya kwanza inapaswa kuwa ya kitaalamu sana.

‎Au iwe na maneno ya Kiswahili kigumu.

‎Au iwe ndefu kama maelezo ya mtihani wa Form Four.

‎HAPANA!

‎Sentensi ya kwanza inapaswa kuwa na kitu kimoja tu HISIA.

‎Ipasue moyo.

‎Iguse akili.

‎Ichokoze curiosity.

‎Ikamate macho.

‎Na iseme, “Usiende popote.”

‎Ukitaka kuandika sentensi ya kwanza inayogusa hisia:

‎Gusa maumivu.

‎Gusa ndoto.

‎Gusa wasiwasi.

‎Gusa ndani ya moyo wake.

‎Mfano?

‎"Unajua uchungu wa kuamka kila siku kwenda kazini, lakini mshahara haukutoshi hata kununua sabuni?"

‎Boom!

‎Msomaji anashtuka.

‎Anajiona humo humo.

‎Anataka kujua zaidi.

‎Anabaki hapo hadi mwisho.

‎Namkumbuka jamaa mmoja aliyenifuata DM.

‎Alikuwa ameandika makala 12.

‎Zote hazina engagement.

‎Alikuwa tayari kukata tamaa.

‎Nikamuuliza, "Sentensi ya kwanza inasema nini?"

‎Akaninukuu:

‎"Katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali, maudhui bora yana nafasi kubwa katika kukuza biashara."

‎Nikamuambia ukweli mchungu:

‎"Bro, hiyo sentensi haina roho."

‎Nikampatia mbinu moja tu:

‎Anze kwa kugusa uchungu wa msomaji.

‎Akaandika tena.

‎Makala yake ikaanza:

‎"Unaweza kuwa na biashara nzuri, lakini kama hakuna anayejua ipo... utaishia kulia kimya kimya."

‎Matokeo?

‎Makala iliwaka moto.

‎Likes, comments, shares zikaongezeka kama mvua ya masika.

‎Ukweli ni huu:

‎Sentensi ya kwanza si sentensi tu.

‎Ni mlango wa hisia.

‎Ni kama kofi la upole usoni  linakufanya usimame na kusema, “Ngoja nisome.”

‎Usichezee mwanzo wa makala yako.

‎Hapo ndipo msomaji anaamua:

‎“Nisome au niache.”

‎Sasa nikuulize...

‎Sentensi yako ya kwanza inafanya kazi hiyo?

‎Au inapita tu kama upepo wa usiku?

‎Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu ujuzi huu adimu ambao haufundishi shuleni,

‎Basi tuma ujumbe *NIFUNDISHE UJUZI ADIMU*

‎Kwenda 0750376891.

‎Karibu.

‎Makala Hii Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection