Copywriting Ni Nini? Na Kwa Nini Inaweza Kukupa Mauzo Kabla Hata Hujapiga SIMU?
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kaka, Dada Yangu… Hebu niambie ukweli…
Umeshawahi kutuma ofa kwenye WhatsApp group, halafu hakuna aliyejibu?
Umeandika post ya biashara, ukaituma hadi kwa mamako, halafu kimya kimya tu?
Uliweka tangazo kwenye status halafu hakuna hata mtu mmoja wa kuulizia bei?
Inauma. Inakatisha tamaa. Inakatisha ndoto.
Lakini unajua tatizo si biashara yako?
Si bidhaa yako.
Si bei yako.
Na wala si bahati mbaya.
Tatizo ni MANENO unayotumia kuuza.
Yaani Wewe Unafanya Kazi Kama Ng’ombe…
Unaamka mapema, unalipia matangazo, unajituma…
Lakini pesa? Haziji.
Wengine wanaposti post moja tu,
Mpaka watu wanaanza kuomba namba ya kutuma hela.
Unashangaa: "Hivi huyu ana nguvu za giza au?"
La hasha!
Ana kitu kinaitwa COPYWRITING.
Copywriting ni nini sasa? Hebu nielewe vizuri.
Copywriting ni sanaa ya kutumia maneno ambayo yanamshawishi mtu achukue hatua.
Iwe ni kununua…
Kudownload…
Kusubscribe…
Au hata kupiga simu.
Ni maneno yanayogusa akili na moyo.
Maneno yanayochoma hisia.
Maneno yanayomlazimisha mtu aseme:
"Naomba niitumie hela sasa hivi!"
Na kama bado hujaelewa… Hebu niweke wazi.
Kuna watu wanafanya copywriting bila hata kujua.
Wanaandika status moja tu,
Halafu wanajaza oda hadi simu yao inagoma.
Wakati huo, wewe unashangaa:
“Hivi huyu alitumia maneno gani?”
“Hii post yake iko tu kawaida, lakini watu wanapagawa nayo.”
Basi acha nikuambie ukweli mchungu:
Maneno uliyotumia hayakumvuta mteja.
Hayakumshawishi.
Hayakumgusa.
Na ndio maana hakuchukua hatua.
Lakini Subiri Kidogo—Habari Njema Ni Hii Hapa:
Copywriting inafundishika.
Inajifunzwa.
Na mtu yeyote anaweza kuimaster.
Unajifunza jinsi ya kuandika:
– Kichwa cha habari kinachovuta macho.
– Sentensi ya kwanza inayoiba umakini.
– Mshiko wa hisia unaomfanya mteja aseme: "Naitaka hii sasa hivi!"
Unajifunza kuongea na mteja kupitia maandishi kama vile mko uso kwa uso.
Na kabla hujampigia, tayari ameshajua thamani ya bidhaa yako.
Amekwishaamua kuwa utanunua.
Ngoja Nikupe Kisa Halisi Kidogo…
Kuna dogo mmoja alikuwa anauza bidhaa moja ya kawaida sana
Sabuni za asili.
Aliwahi kuniambia: “Bro, mimi naandika kila siku, lakini watu wananipotezea.”
Nikamuuliza: “Unaandika nini?”
Akanitumia post zake
Zilikuwa zinaeleza tu faida za sabuni.
Bila hisia. Bila kishawishi. Bila mvuto.
Nikampa somo la haraka Copywriting.
Nikamsaidia kuandika post mpya.
Tulianza na kichwa cha habari kali, tukavuta hisia, tukagusa maumivu ya mteja, tukawasha kiu…
Guess what?
Baada ya siku tatu, alinipigia:
“Bro! Sijawahi kuuza hivi. Simu zinapigwa. Hata wale waliokuwa kimya wamerudi.”
Sasa Hivi Ndio Muda Wako.
Copywriting sio kwa ajili ya watu wachache tu.
Ni kwa mtu yeyote anayehangaika kuuza.
Ni kwa yeyote anayechoka kuomba mauzo.
Ni kwa mtu anayetaka kupiga pesa bila kulazimika kuwasihi watu.
Unaweza kuuza kabla hata hujapiga simu.
Unaweza kuuza kabla hujamaliza sentensi ya pili.
Na yote inaanza na kujifunza jinsi ya kuandika maneno yanayouza.
Unataka nifundishe?
Niandikie tu: "Nataka kujua copywriting"
Kwenda 0750376891.
Na safari ya kuuza bila stress itaanza.
Ukijifunza hii kitu…
Hata ukiwa kimya, watu watanunua.
Na hiyo ndo nguvu ya COPYWRITING.
Karibu.
Mkufunzi Ramadhani Amir
0750376891
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine

Maoni
Chapisha Maoni