🔴 Wateja Wana Sababu 5 Tu Za Kukataa Kununua....
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Na Kama Huzizimi Mapema, Utauza Ndoto Zako Tu!
Wewe ni muuzaji, MJASIRIAMALI au mfanyabiashara?
Huu ndio mfumo wa kukusaidia kuwauzia hata wateja wagumu kuliko wote.
Kumbuka, kazi yako si kuuza tu ni kuzima visingizio kabla havijaota meno.
Unahangaika na wateja.
Unawashawishi kwa nguvu.
Wanakuambia, "Ngoja nifikirie."
Au, "Nitaludi baadaye."
Na hakuna kinacholudi.
Tatizo si bei yako.
Tatizo si bidhaa yako.
Tatizo ni pingamizi ambazo hukuzizima mapema.
"Sina pesa sasa hivi."
"Nimewahi kununua kitu kama hiki, hakikufanya kazi."
"Nitamuuliza mke/mume wangu kwanza."
"Ngoja nifikirie kwanza."
"Si muda mzuri kwangu kwa sasa."
Hizo ni objections tano kuu.
Na kila objection ni bomba la kuzuia hela zako zishuke mfukoni.
Ukikaa kimya, imekula kwako.
Ukijitetea vibaya, wanakosa imani.
Ukizizima mapema... unashinda mapema.
Wauzaji wa kawaida hukimbia objections.
Wauzaji waliobobea huzizima kabla hazijasemwa.
Na hapa ndipo unahitaji kujua hizi tano:
Objection #1: Sina Pesa
✅ Zima mapema kwa kuuliza:
“Unaposema huna pesa, unamaanisha huna kabisa au una vipaumbele vingine kwa sasa?”
Objection #2: Nahitaji Kufikiria
✅ Zima mapema kwa kusema:
“Kama huna swali lolote sasa, kuna uwezekano unafikiri nini hasa kabla ya kusema ndiyo?”
Objection #3: Nitamuuliza Mwenza
✅ Zima kwa kuuliza:
“Je, tukimuita apate maelezo hapa hapa, itakuwa rahisi kufanya maamuzi pamoja?”
Objection #4: Si Muda Mzuri
✅ Zima kwa kusema:
“Niambie, kama huu ndio muda sahihi, ungetaka kuanza lini? Kwa nini?”
Objection #5: Sitaki Kufanya Makosa Tena
✅ Zima kwa kuwapa uthibitisho hai:
“Wengi waliokuwa na hofu kama yako, leo wanashangaa kwa nini walichelewa sana.”
Tumia Mfumo wa Kuzizima Mapema
👉 Kila unapoanza kuwasilisha ofa, sema objections kabla hawajasema.
Unawashangaza.
Unawaamini.
Unawapunguza uoga.
Hii inaitwa: “Pre-framing objections.”
Ni kama kusafisha njia kabla hujapita.
Na matokeo yake?
Unafunga dili mapema. Bila kubembeleza.
. 📚 Hadithi ya Ukweli: Dili Langu la Milioni 5 Lilikimbia kwa Sababu Moja Tu...
Nilikuwa na client mmoja mkubwa.
Nikampelekea ofa ya huduma zangu — branding, copywriting, full funnel.
Akafurahi.
Akasema, “Hii kazi ni nzuri sana. Tutaongea na mke wangu halafu tukujulishe.”
Nikakosea.
Nikakubali kusubiri.
Siku mbili baadaye, sipokei simu.
Wiki ikapita, nikamuona ana-run campaign na jamaa mwingine.
Kilichotokea?
Sikuzima objection mapema.
Ningeuliza, “Je, mkeo ana nafasi ya kuongea leo tukajibu maswali yake moja kwa moja?” — hiyo milioni 5 ingekuwa yangu.
Tangu hapo, najua:
Objection ikishinda, unashindwa.
🔚 Mwisho wa Siku...
Wateja hawakatai kwa sababu hawapendi bidhaa yako.
Wanakataa kwa sababu wana maswali ambayo hujajibu mapema.
Na kazi yako sio kusubiri waulize
Ni kuwatuliza kabla hawajawa na wasiwasi.
📢 Ukijifunza kuzizima objections hizi tano,
utaanza kufunga dili hata kwa wale waliowahi kukukataa!
JIULIZE:
Leo umepoteza dili ngapi kwa sababu hukuzungumzia objections mapema?
Je, unataka mfumo huu kwa kina?
Jiunge na Kozi Ya Copywriting utajifunza kuwauzia hadi watu wagumu kama chuma!
Kujiunga Tuma Meseji "NIUNGE"
Kwenda 0750376891.
Karibu.
Rafiki Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
0750376891.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni